×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Karua awazia kuwasilisha kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki

News

Aliyekuwa Mgombea mwenza wa Azimio Martha Karua amesema anawazia kuwasilisha kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki, kutafuta haki kuhusu kesi waliyowasilisha kupinga matokeo ya urais.

Akizungumza leo hii, Karua ambaye amekariri kuheshimu uamuzi wa Mahakama ya Juu uliodumisha ushindi wa William Ruto, amesema msimamo wake ni wa binafsi ila si wa Azimio.

Karua amefafanua kwamba sababu ya kufikiria kuwasilisha kesi hiyo ni kutaka ufafanuzi zaidi wala si kupinga ushindi wa Ruto.

Karua amesema kwa sasa anasubiri uamuzi kamili kutolewa kuhusu kutupiliwa mbali kwa kesi waliyowasilisha.

Ikumbukwe kisheria, nchini Kenya uamuzi wa Mahakama ya Juu kuhusu kesi za kupinga matokeo ya urais huwa kauli ya mwisho.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week