×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Kamati ya Leba yapendekeza kupunguzwa kwa miaka ya kustaafu

News

Kamati ya Bunge ya Leba sasa inapendekeza kupunguzwa kwa umri wa kustaafu kutoka miaka 60 hadi 55.

Pendekezo hilo linatarajiwa kujumuishwa katika Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Tume ya Huduma za Umma uliowasilishwa na Mbunge wa Embakasi ya Kati Benjamin Gathiru.

Mswada huo unalenga kuweka sheria inayozuia afisa wa umma kuhudumu katika wadhfa wowote kikaimu kwa zaidi ya miezi sita.

Hata hivyo wakati wa mjadala hapo jana wabunge kadhaa wakiwamo wa Kangundo Fabian Muli na Ken Chonga wa Kilifi Kusini walisema kuna haja ya kujumuisha kipengele cha kupunguza umri wa kustaafu kutoka hadi 55 ili kuwapa nafasi watu wengine kuajiriwa.

Ikumbukwe, umri wa kustaafu ulikuwa miaka 55 hadi mwaka 2009 ulipoongezwa hadi miaka 60.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week