Idara ya Upelelezi DCI imeanzisha uchunguzi kufuatia madai ya ulaghai wa mpango wa masomo kwa wanafunzi kutoka Kaunti ya Uasin Gishu waliofaa kusomea nchini Finland na Canada.
Katika taarifa yake jioni hii DCI imesema hatua hiyo inafuatia malalamiko kutoka kwa wakazi wanaodai kulaghaiwa mamilioni ya pesa wakiahidiwa kuwa wanao wangefadhiliwa kusomea nchini humo.