×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Serikali yaanza kutoa chanjo dhidi ya yellow Fever

News

Serikali imeanza rasmi kutoa chanjo dhidi ya homa ya manjano yaani yellow Fevor kwa wakazi wa Kaunti ya Isiolo na Garissa.

Wizara ya Afya imezindua kampeni hiyo leo hii  huku ikilenga hasa maeneo la Merti na Garbatula kwenye Kaunti ya Isiolo na Lagdera, Balambala katika Kaunti ya Garissa ambapo takriban  watu elfu mia saba wanatarajiwa kuchanjwa.

Akizungumza mjini Garissa alipoongoza kampeni hiyo, Kaimu Mkurugenzi Matibabu wa Wizara ya Afya Daktari Patrick Amoth amesema wanaolengwa ni watu wote, kuanzia watoto wa miezi tisa hadi wazee wenye umri wa miaka sitini.

Daktari Amoth amezitaka serikali za Kaunti kuhakikisha kwamba zinashirikiana na maafisa wa afya kufanikisha kampeni hiyo.

Kampeni hiyo imezinduliwa kufuatilia mlipuko wa homa ya Yellow Fever katika kaunti hizo za Garrisa na Isiolo mapema mwaka huu, ambapo watu watatu waliripotiwa kufariki dunia.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week