×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

IEBC yailaumu serikali kufuatia kuzuiliwa kwa maafisa wake JKIA

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, IEBC Wafula Chebukati ameshtumu kukamatwa kwa maafisa watatu wa Kampuni ya  Smartmatic International BV iliyopewa kandarasi na Tume ya Uchaguzi, IEBC ya kuwasilisha mashine za kupigia kura za KIEMS. Maafisa hao walikamatwa hapo jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta. 

Chebukati amethibitisha kukamatwa kwa maafisa hao huku akiitaja hatua ya kukamatwa kwao kuwa ya kuwafedhehesha na ya kulenga kupaka tope kampuni hiyo yenye jukumu kuu la kufanikisha uchaguzi mkuu.

Katika taarifa ya Chebukati usiku wa kuamkia leo amesema kwamba watatu hao walikamatwa walipowasili katika Uwanja wa JKIA kutoka nchini Venezuela.

Walikamatwa licha ya Afisa Mkuu Mtendaji wa IEBC, kuwaelezea maafisa wa usalama kwamba walikuwa humu nchini kutekeleza shughuli ya maandalizi ya uchaguzi mkuu. 

Hata hivyo inadaiwa kwamba watatu hao walikamatwa na nembo za karatasi za uchaguzi za maeneo bunge kadhaa nchini, jambo ambalo IEBC imelikana. Chebukati  sasa anataka watatu hao waachiliwe mara moja akisema kwamba iwapo wataendelea kuzuiliwa huenda hali hiyo ikatatiza maandalizi ya uchaguzi mkuu.

Inaarifiwa kuwa  maafisa wa uchunguzi wanataka kufahami kwa nini stakabadhi hizo za uchaguzi hazikusafirishwa kama mzigo na badala yake kusafirishwa moja kwa moja na watatu hao

Ikumbukwe wakati wa mahojiano na wanahabari siku chache zilizopita, Chebukati na Afisa Mkuu Mtendaji, Marjan Husssein Marjan walitakiwa kutoa maelezo kuhusu namna walivyoafikia kuipa kampuni hiyo ya Smartmatic kandarasi ya kuwasilisha mashine za Kiems ilhali awali imehusishwa na visa vya wizi wa kura katika mataifa mbalimbali kama vile Nigeria na uhalifu wa kimtandao.

Hata hivyo akiitetea IEBC, Marjan alisema kwamba masuala hayo hayakuibuliwa wakati wa kuzichuja kampuni zilizowasilishwa maombi ya kupewa kandarasi ya kuwasilisha vifaa vya uchaguzi.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week