×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Ruto kuhudhuria mdahalo wa wagombea urais tarehe 26 Julai

News

Mrengo wa Naibu wa Rais William Ruto umetoa taarifa kuhusu namna mdahalo wa wagombea wenza wa urais ulivyofanyika wiki hii.

Kupitia taarifa, Mkurugenzi wa Mawasiliano katika kampeni za Ruto Hussein Mohamed amesema kuwa mrengo wao umebainisha kuwa mdahalo huo haikuifanya kipaumbele matakwa ya umma.

Badala yake, Hussein amesema kuwa muda mwingi ulitumiwa na waendesha mdahalo wenye kuangazia masuala binafsi.

Kutokana na hilo, mrengo huo sasa unashinikiza masuala muhimu yanayowaathiriwa Wakenya kuzingatiwa katika mjadala ujao wa urais  Jummane wiki ijayo ambapo imethibitishwa kuwa Ruto atahudhuria .

Taarifa hiyo pia imehusu pale ambapo Ruto atafanyia kampeni yake ya mwisho baada ya mvutano kuibuka baina ya Azimio na Kenya kwanza kuhusu Uwanja wa Nyayo.

Hussein amesema kuwa Ruto atafanya kampeni yake ya mwisho Agosti sita katika Uwanja wa Nyayo licha ya kupokea barua ya kusitisha mkutano huo hata baada ya kufanya malipo.

Kenya Kwanza inaulaumu Azimio kutokana na hatua ya kuzuiwa kutumia uwanja huo huku sasa ikitaka thibitisho kwamba Azimio ilipokea idhini ya kuendesha mkutano wao wa mwisho uwanjani humo.

Suala jingine wanadai ni kwamba Rigathi Gachaua alipewa muda wa dakika 32 kuwasilisha hoja zake huku Martha Karua wa Azimio akipewa 39.

Wanahabari Eric Latiff wa KTNEWS na Yvonne Okwara wa Citizen TV ndio watakaoongoza mdahalo wa wagombea urais utakaowashirikisha Raila Odinga wa Azimio na William Ruto wa Kenya Kwanza.

Mdahalo wa kwanza utakaowashirikisha Prof. George Wajackoyah wa Chama cha Roots na David Mwaure wa Agano utaongozwa na Ken Mijungu wa KTN News na Smitri Vidyarti wa NTV.

Mhariri wa NTV, Joe Ageyo ataongoza midahalo ya uchanganuzi kabla na baada ya midahalo yote miwili. Midahalo hiyo itaanza saa kumi na moja na kuendelea hadi saa nne usiku. Shughuli hiyo itafanyika Julai 26 yaani Jumanne wiki ijayo.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week