×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Tango hukinga saratani na tezi za uzazi ‘Prostrate’

Health & Science
 Vyakula bora vinavyosaidia kupambana na saratani mwilini.

Kwa sababu ugonjwa wa saratani umekuwa tishio au janga la kitaifa nchini Kenya, basi mboga ni chakula ambacho kinasaidia kupunguza uwezo wa kupata ugonjwa huo hatari wa saratani.

Mboga au mabogaa (matango) pia husaidia zaidi kupunguza uwezo wa kupata magonjwa ya macho, kisukari na pia kuongeza kinga mwilini kwajili ya Vitamini A, Vitamini C na Vitamini E iliyo ndani yake.

Matango yana matumizi mengi katika mapishi kuanzia ganda lake mpaka mbegu na hata matawi ya mmea huo pia ina faida zake.

Hutayarishwa upesi kwa kupasuliwa vipande vipande na kuoshwa kisha kuchemshwa au kuokwa ikiwa na maganda yake bila kubambuliwa. Ikiiva pia huliwa hivyo hivyo na maganda yake ukipenda.

Kwa wale hawajui maboga, boga ni tunda la mboga lenye umbo la kibuyu, tunda hili liko katika familia ya Cucurbitaceae. Mboga huwa na rangi ya manjano, machungwa au kijani.

Pia tango ni tunda ambalo huwa na mikunjo kuanzia kwenye shina juu mpaka chini, maboga huwa na kombe au ukipenda ganda nene huku mbegu na nyama ya tunda ikiwa ndani.

Athari za jua kali Wataalam wanasema ulaji wa mboga husaidia ngozi kutoharibika kutokana na jua kali, ni bora kwa zeruzeru ambao huumia sana wakati wa jua kali kando na kinga ya magonjwa mwilini.

Mafuta ya mbegu za tango husaidia kupunguza presha au pumu, mafuta haya ya mbegu za mboga huwa nyekundu na nzito yanapotumika kwa chakula yaweza kusaidia sana watu wenye matatizo ya tezi za uzazi ‘’Prostrate’’.

Mafuta haya pia yana kemikali zinazosaidia kuimarisha mishipa ya ufahamu (neva), pia husaidia kuongeza kuchochea mmeng’enyo wa chakula tumboni.

Mboga zake zina umuhimu tele kwa mwili wa mwanadamu lakini ajabu ni kwamba watu hawajazingatia ulaji wa maboga kama ilivyo kwa matunda mengine. Inashauriwa kwamba badala ya kunywa chai kila siku kwa mkate, mandazi, chapati au kitafunio chochote kile, mtu anafaa kunywa chai kwa maboga angalau mara moja au mbili kwa mwezi.

Hii itamsaidia zaidi kutokana na maambukizi ya magonjwa mengi ya kisasa ambayo yamekuwa tishio. Mboga zina msimu, mwezi wa Januari na huu wa Agosti ni msimu wa mboga, ukienda sokoni sasa utauziwa boga moja kwa kati ya Sh. 50 na Sh. 100 kulingana na ukubwa wake.

Wakati ambao sio msimu wake utapata boga moja lauzwa kwa kati ya Sh. 150 na Sh. 200 kulingana na ukubwa wake pia.

Kuna haja ya kuanza kula vyakula vya kiasili ili kupunguza maambukizi ya magonjwa hatari kama saratani, chakula kama vile maboga ambayo watu wamekuwa wakiona kama chakula kilichopitwa na wakati, inafaa kuliwa zaidi nchini Kenya.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week