×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Uhaba wa madaktari wa kichwa ni hatari kwa ajali za boda boda

Health & Science
 

Uhaba wa madaktari wa kichwa ni hatari kwa ajali za boda boda. [Photo, Standard]

Serikali kuu nchini imehimizwa kuongeza idadi ya madakitari wenye taaluma ya tiba ya majeraha wa kichwa humu nchini.

Himizo hilo limetolewa na dakitari anayehusika na taaluma hiyo ya matibabu ya majeraha ya kichwani katika hosipitali kuu ya ukanda wa pwani Dkt.Benjamin Okanga, akisema kwamba idadi ya madakitari wenye tajiriba hiyo  ni ndogo mno ikizingitiwa kuwa idadi ya wagonjwa wenye majeraha vichwani inazidi kuongezeka kila uchao. 

Katika kikao na waandishi habari kwenye mafunzo kuhusu ukumbusho wa masuala ya upasuaji wa kichwa katika hospitali kuu ya ukanda wa Pwani, Dkt. Okanga amesema kuna haja ya madaktari nchini kupata  ujuzi wa kushughulikia matatizo ya kichwa, ili kuhakikisha uhaba wa wataalam hao unapungua.

“Tuna ukosefu mkubwa wa madakitari wa kushughulikia majeraha ya kichwa nchini  na tunaiomba serikali iwafadhili wale madakitari ambao wanataka kusomea taaluma hii, ili idadi iongezeke na kuwasaidia wagonjwa ambao wako mashinani,” akasema Dkt.Okanga.

 Aliongeza na kusema hosipitali nyingi za mashinani zinakosa huduma hizo za kuangalia majeraha ya kichwa kutokana na kuongezeka kwa ajali katika sehemu mbali mbali nchini.

Amesema wagonjwa wengi ambao wanaathirika na ajili na kuumia vichwa huwa ni waendeshaji wa bodaboda ambao huendesha pikipiki bila kutumia kofia za kujikinga wakati ajali zinapotokea barabarani.

Dkt. Okanga alizidi kuhumiza kwamba endapo madaktari zaidi watapata  mafunzo hayo, huenda ikasaidia pakubwa kuokoa maisha ya watu haswa walioko mashinani, huku akisema hatua hiyo itapunguza gharama kwaa majeruhi kusafiri kwenda hospitali za mbali kwa matibabu.

“Watu wengi ambao wanaathirika na kuumia kwa vichwa, mara nyingi ni waendeshaji pikipiki na wanapopata ajali hulazikia kuletwa hadi katika hospitili hii kuu ya ukanda wa pwani kwa sababu hosipitali nyingi za mashinani hazina madakitari wa kushughulikia majeraha ya kichwa ,” akasema Okanga.

Wakati huo huo Dkt. Oganga ameiomba serikali kuu kuweka mikakati kabambe ya utekelezaji wa sheria barabarani huku akisema hiyo ndiyo njia bora itakayopunguza ajali zinazosababisha maafa mengi humu nchini.

Kadhalika amezitaja sheria za Michuki kuwa bora akisema kuwa wakati zilipokuwa zikitumika hakukutokea visa vingi vya ajali nyakati hizo ikilinganisha na hivi sasa, huku akiwataka madereva kutii sheria za barabarani.

Kuwekwa kwa mishipi katika magari ya usafiri wa umma pamoja na waendeshaji pikipiki kutumia kofia za kujikinga huenda kukapunguza ajili barabarani ambazo zitasaidia kupungua visa vya wagonjwa ambao wanaumia vichwa wakati wa ajali humu nchini.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week