×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Polisi 4 waliohukumiwa kwa kumuua raia wa Uingereza Alexander Manson, waachiliwa

News

Mahakama ya Rufaa jijini Mombasa imewaachilia huru mafisa wote wanne waliopatikana na hatia ya mauaji ya raia wa Uingereza, Alexander Monson.

Tarehe 15 mwezi Novemba Mahakama Kuu jijini Mombasa iliwafunga jela wanne hao baada ya kuwapata na hatia ya kumuua bila kukuudia Alexander aliyepatikana amefariki dunia katika seli ya Kituo cha Polisi cha Diani kwenye Kaunti ya Kwale mwaka 2012.

Akitoa hukumu hiyo Jaji Erick Ogola alisema kwamba uamuzi huo ulifuatia ushahidi uliowasilishwa mahakamani uliothitisha wanne hao kuhusika katika mauaji hayo.

Mafisa hao Naftali Chege, Charles Wangombe Munyiri, Bakari Muluma na John Pamba walihukumiwa vifungo tofauti jela.Chege alihukuwa miaka 15 jela, Munyiri miaka 12, Buluma miaka 9 huku huku Pamba akahukumiwa miaka 12 jela.

Monson aliyekuwa na miaka 28 alipatikana amefariki baada ya kukamatwa kwa kile polisi walidai alipatikana akivuta bangi wakati wa usiku huko Diani.

Kwa mjibu wa Ogola ushahidi ulithibitisha kwamba mafisa wa polisi walimukelea kosa hilo kwani alikuwa buheri wa afya alipokamatwa na alifariki baada ya kuteswa alipokuwa akizuiliwa.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week