×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Sampuli ya magonjwa yanayoathiri viungo mwilini

Mwanadamu anakabiliwa na kila sampuli ya magonjwa. Kuna magonjwa yanayotokana na aina ya kazi tunazofanya, na kuna magonjwa ya kimaumbile ambayo humsibu mwanadamu.

Yapo magonjwa ambayo yanaathiri viungo hasa kuanzia kiunoni kuteremka chini, na mengi ya magonjwa haya yanatokana na kuvipa viungo mzigo mkubwa wa kubeba.

Kuna wafanyikazi ambao kutokana na kazi zao inawabidi kuchuchumaa kwa muda mrefu, kupinda maungo hasa miguu kwa muda mrefu, na kuna kazi nyingine huleta madhara ya viungo kuumia kazini kwenye michezo, kwenye ajali, kuanguka na kadhalika.

Baadhi ya magonjwa hutatiza utendaji wa kazi wa mhusika na hata kumpotezea nguvu za utendakazi pia. Madhara anayopata mwanadamu katika viungo vya kuanzia kiunoni nadi kwenye wayo ni pamoja na kupata maumivu ya kiuno, nyonga, miguu na magoti na kwa kawaida hutokana na kutumiwa kupita kiasi kwa viungo hivyo.

Wafanyikazi mara nyingi hulalamika kuumwa na viungo hivyo na kupata ganzi hata bila ya kupatikana kwa magonjwa yoyote wanayougua. Magonjwa yanayosababishwa na madhara makubwa yanayoletwa na matukio ya ghafla kama vile ajali si kawaida kutokea na kusababisha madhara hayo, lakini wanariadha na wanajeshi hukabiliwa na aina hii ya madhara kwa hivyo ni bora kuwafahamisha wahusika mapema.

Ushahidi wa kisayansi unaeleza kwamba kuna magonjwa kadha yanayoathiri viungo vya chini kuanzia kiunoni, ambayo yana uhusiano na kazi, magonjwa kama vile arthritis ya kiuno na magoti na pia kuna magonjwa ambayo yanajulikana kwa lugha za kitaalam kama vile knee bursitis, meniscal lesions/tears na magonjwa mengine yanayoshika sehemu za chini za miguu.

Kwa maelezo mafupi ya magonjwa haya ni kama ifuatavyo:- Ugonjwa unaoitwa Osteoarthritis (OA) ni ugonjwa ambao unapokupata huwa hautibiki kwa urahisi na unaendelea kuleta madhara makubwa. Ni ugonjwa unaoshika kiuno nyonga na uti wa mgongo.

Madhara hayo hukupata wakati sehemu ya maungo yanayofunika viungo hivyo yanapoharibika ama kuisha. Magonjwa haya ya nyonga yanapatikana zaidi kwa wanaume kuliko kwa wanawake, na wakulima wako katika hatari kubwa ya kuathirika kwa asilimia kubwa kwa sababu ya ugonjwa huu.

Kundi jingine la wafanyi kazi ambalo limo katika hatari ya kupata magonjwa hjaya ni pamoja na wachimba migodi, wafanyikazi wa kutengeza sakafu kama vile wanaoweka “tile” majumbani, na wanaofanya kazi za kusafisha sakafu.

Knee bursitis ni ugonjwa ambao umebandikwa majina mengine kama vile ugonjwa wa wachimba madini, ugonjwa wa waandalizi wa mazulia, na ugopnjwa wa magoti wa wafanyikazi wa nyumbani. Ugonjwa huu husababishwa na kuchuchumaa mara kwa mara au kufanya shughuli ambazo zitalifanya goti kulemewa na uzito mara kwa mara.

Wafanyikazi wanaopata ugonjwa huu mara nyingi hulalamika kuhusu kuvimba kwa magoti na sehemu za goti kuwa laini, na kupungua kwa utumiaji wa goti lako kwa sababu ya maumivu hivi kwamba haliwezi kuwenda huku na huku, na ngozi ya sehemu za goti kuwa ngumu.

Pia kuna ugonjwa wa ngozi ya goti kuwa nzito unaojulikana kama Beat knee au hyperkeratosis. Ugonjwa huu unasababishwa na shinikizo kubwa la goti, yaani kulipa kazi za uzito mkubwa.

Huu ni ugonjwa mkubwa wa bursitis na ni ugonjwa wa kawaida kwa wale wanaojishughulisha na kazi zinazolipa goti shinikizo kubwa la kikazi kama vile kupiga magoti na kuchuchumaa.

Ugonjwa mwingine ni wa Meniscal lesions/ tear damage ambao unahusu kupinda au kunyongeka kwa goti wakati mtu anapobeba mzigo wenye uzito mkubwa. Mzigo unapokuwa mzito unaweza kusababisha madhara kwenye goti na kusababisha mipasuko ya sehemu za goti.

Madhara hayo yana uwezo wa kusababisha ugonjwa wa goti kuwa mbaya zaidi na hatua za tahadhari zinapaswa kuchukuliwa mapema iwezekanavyo. Madhara mengine ya goti yanajulikana kama Stress fracture magonjwa haya yanasababishwa na kuyapa magoti mshindo wa kuendelea ambao husababisha mifupa ya miguu kupasuka kidogo kidogo.

Magonjwa haya huwapata zaidi wanaofanya kazi za kijeshi kutokana na mazoezi yao ya kutembea kwa kukanyaga kwa mshindo mkubwa. Magonjwa haya yanapatikana zaidi kwa vikosi vya kijeshi na wanariadha, hasa wale wanaoshiriki riadha za mbio ndefu.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week