×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Gachagua awasilisha rufaa kupinga kurejesha shilingini milioni 202

Living

Mahakama ya Rufaa sasa ndiyo itakayobaini kuhusu madai ya ufisadi wa shilingi milioni 202 yanayomkabili Mgombea mwenza wa Chama cha UDA Rigathi Gachagua.

Gachagua ambaye pia ni Mbunge wa Mathira amewasilisha Rufaa akitaka uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumwagiza kurejesha fedha hizo kwa serikali ubatilishwe.

Kupitia wakili wake Kioko Kilukumi, Gachagua anadai kwamba hakupewa muda wa kujitetea kabla ya uamuzi kuhusu fedha hizo kutolewa. Aidha anaitaka Mahakama kuiagiza Mamlaka ya Kurejesha Mali ya Umma kokama kuzuia fedha zake zilizo katika akunti ya benki ya Rafiki MICRO-finance hadi kesi dhidi yake itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Alhamisi iliyopiya Jaji wa Mahakama Kuu Esther Maina alimwagiza Gachagua kuzirejesha fedha hizo kwa serikali kwa kuwa alizipata kupitia njia ya ufisadi. Mahakama aidha iliamua kuwa Gachagua alidanganya kwamba alizipata fedha hizo kupitia zabuni alizopewa na taasisi mbalimbali za serikali kwani hakuwasilisha ushahidi kuthibitisha madai hayo.

Uamuzi huo wa mahakama umeendelea kumpaka tope mgombea mwenza huyo wa William Ruto huku washindani wao wakiidi kuutumia kuwa chambo katika kampeni zao kwani wamekuwa wakimshinikiza kuondoka kinyanganyironi wakisema hafai.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles