Aliyekuwa Mgombea mwenza wa Azimio Martha Karua amesema anawazia kuwasilisha kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki, kutafuta haki kuhusu kesi waliyowasilisha kupinga matokeo ya urais.
Akizungumza leo hii, Karua ambaye amekariri kuheshimu uamuzi wa Mahakama ya Juu uliodumisha ushindi wa William Ruto, amesema msimamo wake ni wa binafsi ila si wa Azimio.
Karua amefafanua kwamba sababu ya kufikiria kuwasilisha kesi hiyo ni kutaka ufafanuzi zaidi wala si kupinga ushindi wa Ruto.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.