×
App Icon
The Standard e-Paper
Informed Minds Prefer The Standard
★★★★ - on Play Store
Download Now
×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

JSC Yakosolewa kwa Kutojibu Masuali Kuhusu Uteuzi wa Jaji Mkuu Mpyaa

Living

Na, Beatrice Maganga

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Nchini, Yash Pal Ghai ameishtaki Tume ya Huduma za Mahakama JSC kwa kutoziweka bayana sababu za kukatowaorodhesha baadhi ya watu waliowania nyandifa kwenye idara ya mahakama zilizotangazwa hivi majuzi. Kupitia wakili wake Waikwa Wanyoike, Ghai amesema kuwa licha ya kuiandikia barua tume hiyo mnamo Julai 14, hadi sasa hajapokea maelezo. Amesema hatua hiyo inakiuka katiba inayosisitiza umuhimu wa uwazi vilevile uongozi bora serikalini. Ghai pamoja na mkenya kwa jinar Samwel Muhochi wameitaka mahakama kuiagiza JSC kuweka wazi sababu hizo kwa umma. Mahakama imeitaja kesi hiyo kuwa ya dharura na kuagiza isikilikwe siku ya Ijumaa wiki hii. Tume hiyo ilizitangaza nafasi za Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na Jaji kwenye mahakama hiyo mnao Juni kumi na saba. Tume hiyo kisha iliyaorodhesha majina ya wawaniaji wa nafasi hizo kati ya Juni 14 na 21 kabla ya kuwateua baadhi yao. Msomi Makau Mutua ni miongoni mwa waliotemwa kwa wanaowania nafasi ya Jaji Mkuu. Walioteuliwa wataanza kuchujwa Agosti 29 hadi Oktoba 7.

 

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week

.

Similar Articles

.

Recommended Articles