×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Mawaziri wateule kuhojiwa kuanzia Jumatatu

Living

Shughuli ya kuwahoji mawaziri wateule inaanza rasmi Jumatatu huku kizungumkuti kikiwa kimezingira uteuzi wa Musalia Mudavadi kuwa Mkuu wa Mawaziri. Katika ratiba ya mahoajiano hayo yatakayoanza Jumatatu hadi Jumamosi ijayo Mudavadi ndiye ameratibiwa kufika wa kwanza, hata hivyo, kabla ya kuhojiwa Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetangula atasubiriwa kutoa mwelekeo kuhusu nafasi hiyo.

Wiki iliyopita Spika Wetangula alisema atatoa mwelekeo huo Jumatatu asubuhi kabla ya shughuli ya kuanza kuwahoji mawaziri wateule kuanza mwendo wa saa tatu. Hatua hii inafuatia mvutano maswali yaliyoibuliwa na upande wa wachache bungeni kuhusu nafasi aliyotengewa mudavadi ukisema haitambuliki kikatiba.

Alhamisi iliyopita mkutano ulioitishwa na Spika Wetangula kuweka mikakati ya kuwahoji mawaziri ulitibuka, -utata ukiwa wadhfa wa Mudavadi. Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Opiyo Wandayi alimtaka Spika kuelezea iwapo Bunge linastahili kumhoji Mudavadi kwa wadhfa huo na kwa misingi ipi. Wandayi alisema katiba imeweka bayana nafasi za maafisa wa umma kuanzia kwa Rais, Naibu wa Rais, Mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akisema wadhfa wa mkuu wa makatibu haupo kikatiba.

Baada ya Mudavadi atakayefuata ni aliyekuwa Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi aliyeteuliwa katika wadhfa wa Mwanasheria Mkuu wa serikali kisha Mbunge wa Garissa mjini Adan Duale ambaye ni Waziri Mteule wa Ulinzi. Baadaye Waziri mteule wa Mashauri ya Nchi za Kigeni Alfred Mutua atafuta na Mbunge wa Kandara Alice Wahome ambaye ni Waziri mteule wa maji atafunga ratiba ya Jumatatu.

Jumanne Profesa Kithure Kindiki ambaye ni Waziri Mteule wa Masuala ya Ndani ya Nchi atahojiwa wa kwanza, akifuatwa na mwenzake wa Fedha Profesa Njuguna Ndungu, Aisha Jumwa wa Huduma za Umma naJinsia atakuwa wa tatu, baadaye Davis Chirchir wa Kawi kisha Mosea Kuria wa viwanda ndiye atakayekuwa wa mwisho siku ya Jumanne.

Jumatano ataanza Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen wa Uchukuzi, atafuatiwa na Soipan Tuya wa Mazingira, Mwenzake wa Utalii Peninah Malonza, atafuata Zacharia Mwangi Njeru wa ardhi atahojiwa siku hiyo vile vile Susan Nakhumicha Wafula, Health wa Afya

Alhamisi vikao hivyo vitachukua mapumziko kupisha sherehe za mashujaa ambayo itakuwa siku ya mapumziko ya kitaifa na kurejelewa Ijumaa ambapo Mithika Linturi aliyeteuliwa katika wizara ya kilimo atafungua chamvi. Wa pili atakuwa Eliud Okech Owalo, wa Habari, mawasiliano na masuala ya Kidijitalii, Ezekeil Machogu wa Elimu atafuata, kabla ya Ababu Namwamba wa Michezo kuhojiwa. Atakayefunga orodha ya Ijumaa ni Rebecca Miano na Afrika Mashariki na Maeneo Kame.

Jumamosi itakuwa zamu ya Waziri mteule wa viwnada Simon Chelugui, ambaye atafuatiwa na Salim Mvrya wa Uchimbaji madini na raslimali za majini, kisha Florence Bore, wa Leba kabla ya Mercy Kiiru Wanajau, ambaye ni katibu mteule wa Baraza la Mawaziri kuhojiwa wa mwisho.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles