Shughuli ya kuwahoji mawaziri wateule inaanza rasmi Jumatatu huku kizungumkuti kikiwa kimezingira uteuzi wa Musalia Mudavadi kuwa Mkuu wa Mawaziri. Katika ratiba ya mahoajiano hayo yatakayoanza Jumatatu hadi Jumamosi ijayo Mudavadi ndiye ameratibiwa kufika wa kwanza, hata hivyo, kabla ya kuhojiwa Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetangula atasubiriwa kutoa mwelekeo kuhusu nafasi hiyo.
Wiki iliyopita Spika Wetangula alisema atatoa mwelekeo huo Jumatatu asubuhi kabla ya shughuli ya kuanza kuwahoji mawaziri wateule kuanza mwendo wa saa tatu. Hatua hii inafuatia mvutano maswali yaliyoibuliwa na upande wa wachache bungeni kuhusu nafasi aliyotengewa mudavadi ukisema haitambuliki kikatiba.
Alhamisi iliyopita mkutano ulioitishwa na Spika Wetangula kuweka mikakati ya kuwahoji mawaziri ulitibuka, -utata ukiwa wadhfa wa Mudavadi. Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Opiyo Wandayi alimtaka Spika kuelezea iwapo Bunge linastahili kumhoji Mudavadi kwa wadhfa huo na kwa misingi ipi. Wandayi alisema katiba imeweka bayana nafasi za maafisa wa umma kuanzia kwa Rais, Naibu wa Rais, Mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akisema wadhfa wa mkuu wa makatibu haupo kikatiba.
Facts First
Unlock bold, fearless reporting, exclusive stories, investigations, and in-depth analysis with The Standard INSiDER subscription.
Already have an account? Login
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.