Naibu Gavana wa Kakamega Ayub Savula anadai kuwa yeye ana mamlaka sawa na Gavana Fernandes Barasa waliochaguliwa naye kupitia chama cha ODM.
Kulingana na Savula, Serikali ya Kaunti ya Kakamega imegawanywa sehemu mbili huku yeye akiongoza mrengo mmoja na Barasa mrengo mwingine.
Katika nafasi za mawaziri wa kaunti, Savula anasema walielewana na Barasa kwamba yeye atateua nusu ya mawaziri.
Kutokana na hilo, Savula sasa hataki kutambuliwa kama Naibu gavana badala yake anapendekeza kuitwa gavana mwenza yani Co-govenor wa Kakamega.
Jumapili, Savula alidai kwamba alishurutishwa kumuunga mkono Raila Odinga wa chama cha Muungano wa Azimio, katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9 na kwamba sasa anamuunga mkono William Ruto ambaye anasubiri kuapishwa kuwa rais wa tano wa Kenya.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.