Shughuli ya usambazaji karatasi za kupigia kura ya ugavana katika Kaunti ya Mombasa imeanza huku mipango yote ikikaribia kukamilika.Mapema leo hii masanduku ya kupigia kura yalifunguliwa ili kuthibitisha karatasi hizo inatekelezwa chini ya uangalizi wa maajenti wa wawaniaji wote 7 wa Ugavana wa Mombasa pamoja na wawaniaji wenyewe.
Baadaye wasimamizi wa vituo vyote 1,037 pamoja na manaibu wao watakabidhiwa vifaa hivyo vya kupigia kura.
Jumla ya wapigakura 641,000 katika Kaunti ya Mombasa wanatarajiwa kujitokeza kushiriki uchaguzi huo utakaofanyika kesho Jumatatu tarehe 29.Wawaniaji wanaomezea mate wadhifa wa Ugavana wa Mombasa ni Hezron Awiti wa VDP, Abdulswamad Sheriff Nassir wa ODM, Hassan Omar wa UDA, William Kingi wa PAA, Kitsao Daniel Munga ambaye ni mgombea huru, Makazi Shaffi Mwaganda wa Chama cha UPIA na Omari Said Abdalla wa Chama cha Usawa Kwa Wote.
Facts First
This story continues on The Standard INSiDER. Subscribe now for unfiltered journalism that holds power to account.
Already have an account? Login
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.