Shughuli ya kuwaapisha wawakilishiwadi imeendelea kwenye mabunge ya kaunti nchini Kenya baada ya kuanza Jumatatu.
Shughuli hiyo itafuatiwa na uteuzi wa viongozi mbalimbali wa mabunge ya Kaunti wakiwamo maspika.
Katika Kaunti ya Trans Nzoia, shughuli hiyo imekamilka ambapo wawakilishiwa wadi 33 wameapishwa, 25 waliochaguliwa na 8 walioteuliwa na vyama.
Uapisho huo umeendeshwa na Karani wa bunge hilo Moses Lubao.
Aidha wawakilishi waid 39, 27 waliochaguliwa na 12 maalumu wameapishwa katika Kaunti ya Siaya.
Jumatatu, wawakilishi wadi wa Nyamira waliapishwa na kumchagua aliyekuwa Mwakilishiwadi wa Manga, Enock Okero kuwa spika mpya.
Nafasi hiyo awali ilishikiliwa na Moffat Teya.
Kuapishwa kwa wawakilishiwadi kumefanyika wakati vyama vya watu wenye ulemavu vimepinga uteuzi wa wawakilishiwadi maalumu kwa madai ya kubaguliwa kwa walemavu.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.