×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Wakenya watamkumbuka vipi Rais Kenyatta anapostaafu?

Living

Rais Uhuru Kenyatta anapostaafu rasmi Jumanne, atakumbukwa kwa rekodi anayoacha kukiwamo kuwa rais wa kwanza kutekeleza kikamilifu katiba ya mwaka wa 2010.

Rekodi ya Kenyatta imejikita zaidi katika miundomsingi ya ujenzi wa barabara na reli ya kisasa ya SGR, iliyogharimu shilingi bilioni 500.

Aidha, Kenyatta ndiye aliyetekeleza ugatuzi ambapo alitumia shilingi trilioni 3 kuwezesha kifedha kaunti 47.

Vilevile, Kenyatta atakumbukwa kwa kuanzisha Mtalaa wa Elimu ya Umilisi CBC, noti mpya na sarafu za shilingi za Kenya, Vituo vya Huduma pamoja na Kadi ya Huduma Namba, kuimarisha usambazaji wa umeme kwa asilimia 71.4, kubadili sare za polisi, na kutoa hatimiliki za mashamba takribani milioni sita.

Alipochukua hatamu za uongozi, Pato la Taifa GDP lilikuwa shilingi trilioni 5.31 ambapo ameongeza hadi trilioni 12.09.

Hata hivyo, anastaafu akiacha Kenya ikiwa na deni la umma la shilingi trilioni 8. 47 kulinganisha na Hayati Mwai Kibaki ambaye aliacha deni la shilingi trilioni 1.6.

Anapostaafu, Kenyatta atalipwa mshahara jumla wa shilingi milioni 39.6, fedha ambazo hazitatozwa kodi.

Pia, atakuwa akilipwa shilingi milioni 1.32 za pensheni ya kila mwezi, pamoja na marupurupu ya shilingi 200,000 kwa burudani, makazi, ofisi, magari, mafuta na huduma za matibabu kutoka kwa serikali.

Aidha, Kenyatta na mkewe Bi, Margret Kenyatta watapewa pasipoti za kidiplomasia na marupurupu ya usafiri wa ndani na kimataifa ya hadi safari nne kwa mwaka kwa mujibu wa Sheria ya Manufaa ya Kustaafu ya Rais mwaka 2003

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles