Maafisa wa Idara ya Upelelezi DCI katika Kaunti ya Kiambu wanachunguza kisa cha kushangaza ambapo msichana wa miaka 15 anadaiwa kuwaua ndugu zake watatu, pamoja na binamu yake katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Inaarifiwa kwamba msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza, amekiri kutekeleza mauaji hayo katika kituo cha Polisi cha Kikuyu, ambako anaendelea kuzuiliwa huku uchunguzi ukiendelea.
Taarifa ya polisi inasema baba wa msichana huyo alijiwasilisha katika Kituo cha Polisi cha Kikuyu akiwa amechanganyikiwa baada ya kumshuku mwanawe kwa tuhuma za mauaji.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.