×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Maraga awasihi wanasiasa kutoiingilia mahakama

Living

Na, Beatrice Maganga Maraga awasihi wanasiasa kutoiingilia mahakama Jaji Mkuu, David Maraga ametoa wito kwa wanasiasa  kujiepusha na mienendo yenye uwezo wa kuhitifaliana na utendakazi wa majaji. Katika kikao na wanahabari, Maraga ametoa mfano wa kisa ambapo Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa, Adan Duale alimkosoa hadharani jaji George Odunga kuhusu maamuzi mbalimbali ambayo amekuwa akifanya. Aidha amekitaja kisa cha Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake, William Ruto kudai kwamba upinzani ulikuwa ukishirikiana na mahakama kuhakikisha uchaguzi mkuu unaahirishwa kupitia kesi mbalimbali zilizowasilishwa mahakamani. Maraga aidha amesema kila jaji ana uhuru wa kufanya maamuzi katika kesi mbalimbali zilizo mbele yake bila shinikizo la aina yoyote. Aidha amesisitiza kwamba idara ya mahakama i tayari kuzishughulikia kesi mbalimbali zitakazowasilishwa mbele yake kuhusu uchaguzi mkuu.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles