Na, Beatrice Maganga/ John Mbuthia Rais asema hakuona umuhimu wa kuhudhuria mjadala wa urais Siku moja baada ya kukosa kuhudhuria mjadala wa urais, Rais Uhuru Kenyatta leo hii ameendeleza kampeni kwenye Kaunti za Murang'a na Nyeri huku akichukua fursa hiyo kufafanua sababu za kutohudhuria mjadala huo. John Mbuthia ameifuatilia ziara hiyo ya Rais na hii hpa taarifa yake. Akihutubu katika eneo la Mukurweni ambalo hakulizuru awali wakati wa ziara yake siku chache zilizopita, Rais Kenyatta amesema alikosa kuhudhuria mjadala kwa kuwa haukona haja ya kufanya hivyo akisema maendeleo aliyowafanyia wananchi yako bayana Uhuru ambaye amesema alimtazama Raila katika runinga wakati wa mjadala huo, amemshtumu kwa kusema hakuwa na mamlaka ya moja kwa moja ya kukabili ufisadi alipokuwa katika serikali ya mseto. Rais Kenyatta aidha hakukosa kuvishtumu vyombo vya habari akisema havijakuwa vikimuunga mkono tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2013.Rais Kenyatta ameendeza ziara maeneo ya Tetu na kuwaahidi wakazi kwamba atabuni kata mpya eneo hilo. Katika Eneo Bunge la Othaya, Rais ameahidi kufunguliwa kwa hospitali ya Rufaa ya Othaya Februari mwaka ujao huku huduma za akina mama kujifungua bila malipo zikiendelea kuboreshwa. Naibu wa Rais, William Ruto ambaye ameendeleza kampeni kwenye kaunti za Vihiga na Kakamega kwa upande wake ameyakosoa madai ya Raila kuwa kuna njama ya kuwahusisha maafisa wa usalama katika kufanikisha udanganyifu wakati wa uchaguzi mkuu.
Rais asema hakuona umuhimu wa kuhudhuria mjadala wa urais
Living
By | 8 years ago | 1 Min read
.
Trending Now
- Woman gives births during Beyond Zero race, names baby girl after First Lady
- This hairstyle is all a woman needs to stay corny and classy for the hot weather
- Dwyane Wade and Gabrielle Union join transgender daughter, Zaya, for her red carpet debut
- Men have a critical role to play in breastfeeding during COVID-19 pandemic
- The opposite of weddings - Top ten reasons for divorce in Kenya
- Nutritionist urges people not to diet in new year and says to 'eat normally' instead
- 'I live for myself': Why Ainam Chamere Ashley chose tubal ligation at 24
- What women like in bed and good manners they expect after sex
- LSK, ICJ and three scholars join as friends of the court
- Social norms hinder uptake of contraceptives among youth
.
Popular this week
- Easy recipe: Walnuts cheesy kunafa
- Playing favourites: The 'golden child' of the family
- How to report a superior without risking your job
- Quiet strength of mothers raising kids with special needs
- Delicate dance: What reciprocity really looks like in relationships
- Elevate your graphic T-shirt into a fashion statement
- Fathers must help kids discover talent
- Why Kisiis unapologetically roast ‘witches’
- TV hunk Nick Mutuma shows off new model girlfriend at Nairobi Fashion Week
- Why married women cheat 'smarter' than men
.
Similar Articles
.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.