×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

IEBC yawataka wawaniaji nyadhifa za kisiasa kuzingatia sheria

Living

Na, Beatrice Maganga Zikiwa zimesalia siku 76 kabla ya uchaguzi mkuu ujao, Tume ya Uchaguzi, IEBC imetishia kuwafungia nje wawaniaji wa urais ambao hawatazingatia sheria za uchaguzi. Tume hiyo imesema itafuata sheria za uchaguzi kikamilifu wakati wa kuwachuja wawaniaji hao na kuwataka wasioridhishwa na baadhi ya matakwa ya kuwania wadhifa huo kurejelea kifungu cha sita cha katiba kuhusu maadili na uongozi.   Akizungumza wakati wa mkutano baina ya Tume ya Uchaguzi, IEBC na wawaniaji urais, Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati amesema wanaolenga urais ni lazima wahakikishe majina watakayowasilisha kwa tume ya wanaowaunga mkono ni ya wanachama wa vyama vyao huku wawaniaji huru wakitakiwa kuwasilisha majina ya wale ambao si wanachama wa chama chochote cha kisiasa.  Kauli ya Chebukati ilitokana na hatua ya baadji ya wawaniaji urais waliohudhuria mkutano huo kulalamikikia mahitaji kadhaa ya kuwania urais likiwmo la  kuwataka kuwasilisha idadi fulani ya saini za wanaowaunga mkono. Abduba Dida ambaye ni Mwaniaji urais kupitia Chama cha Tunza Coalition alilalamikia baadhi ya matakwa hayo. Wakati uo huo, Chebukati amesema dosari za majina zilizopo katika orodha ya wawaniaji wa nyadhifa za kisiasa iliyochapishwa hazikutokana na tume. Chebukati amesema orodha iliyochapishwa ni sawa na iliyotolewa kwa vyama vya kisiasa japo amesema dosari hizo zinaweza kurekebishwa. Rais Uhuru Kenyatta anayelenga kuwania awamu nyingine ya uongozi pamoja na mgombea wa Muungano wa NASA, Raila Odinga hawakuhudhuria mkutano huo japo walituma wawakilishi. Wawaniaji wengine wa urais waliohudhuria ni  Ekuru Autok, Joseph Nyagah, Nazlin Umar, Solomon Gichira, Michael Waweru, Michael Orenge, Eliud Kiriara, Japhet Kavinga, Peter Osotsi, David Munga, Erastus Nyamera na Stephen Awoko.

 

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles