×
App Icon
The Standard e-Paper
Informed Minds Prefer The Standard
★★★★ - on Play Store
Download Now
×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Viongozi watofautiana kuhusu idadi ya waliofariki kutokana na makali ya njaa

Living

Na Carren Ome na Suleminan Yeri

Huku Wakenya kwenye sehemu mbalimbali nchini wakikabiliwa na makali ya njaa, chakula kilichonunuliwa na serikali ya Kaunti ya Samburu na kusambaziwa wakazi, kimetajwa kuwa si salama kwa matumizi ya binadamu. Zaidi ya magunia elfu nane yametajwa kuwa si salama baada ya kufanyiwa uchunguzi katika maabara ya serikali. Kwa mujibu wa Gavana wa Samburu Moses Lenolkulal, magunia hayo yaliigharimu serikali yake shilingi milioni 11.5. Gavana Lenolkulal anashinikiza kuchukuliwa hatua kwa maafisa wa Bodi ya Nafaka na Mazao, NCPB kwa kuiuzia serikali yake mahindi hayo. Hata hivyo, Meneja wa NCPB eneo la Maralal Kipng'etich Mutai amekana taarifa hizo akisema hawajapokea taarifa rasmi kutoka maabara ya serikali. Gavana huyo amesema wakazi wengi wanakabiliwa na hatari ya kuangamia kutokana na makali ya njaa huku akiongeza kuwa wamelazimika kuitegemea serikali ya kitaifa kwa chakula cha msaada. Kwa mujibu wa mamlaka ya kushughulikia ukame nchini zaidi ya watu elfu hamsini na nne kwenye maeneo ya Samburu, Magharibi na Samburu Kaskazini wanakabiliwa na baa la njaa. Wakati uo huo, Serikali imesema imerekodi kisa kimoja pekee cha kifo kilichosababishwa na ukame licha ya madai kuwa watu kumi wamefariki dunia kutokana na makali ya njaa. Msemaji wa Serikali Erick Kiraithe amesema kisa hicho kimetokea Kilifi na kuapa kwamba serikali inafanya kila iwezalo kuzuaia vifo. Hata hivyo amesema ukame utashuhudiwa hadi katika ya mwaka ujao

Kiraithe aidha amewaonya vikali machifu na maafisa wa kaunti watakaopatikana wakiuza chakula cha msaada akisema wataachishwa kazi na kufuguliwa mashtaka. Juma lililopita Mbunge wa Lagdera, Mohamed Shidiye alisema takriban watu saba wamefariki dunia kutokana na makali ya njaa kwenye Kaunti ya Garissa.

 

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles