Na, Carren Omae
Raila apendelewa na wengi akilinganishwa na Kalonzo na Wetangula
Huku mvutano kuhusu suala la ni nani atakayepeperusha bendera ya Muungano wa CORD wakati wa uchaguzi mkuu ujao ukiendelea, imebainika kwamba Kinara wa muungano huo Raila Odinga anaungwa mkono na Wakenya wengi akilinganishwa na vinara wenza, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula. Kulingana na Utafiti wa kampuni ya Ipsos Synovate, asilimia 46 ya Wakenya wana imani na Raila akilinganishwa na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na Seneta Moses Wetang’ula wa Ford-Kenya, ambao wana asilimia 38 kila mmoja. Asilimia 28 ya Wakenya waliohojiwa wanasema Raila anaweza kukabili ukabila, alisimiia 30 wanasema anaweza kukabili ufisadi huku asilimia 29 wakisema ana uwezo wa kuleta maendeleo. Lakini ni asilimia 3 pekee ya Wakenya ndio wanaohisi Kalonzo anaweza kukabili ukabila na kuleta maendeleo. Vilevile ni asilimia 2 pekee wanaohisi Wetangula anaweza kukabili ufisadi huku asilimia 3 wakisema anaweza kuleta maendeleo. Utafiti huo uliofanywa kati ya Juni 4 na 18, hata hivyo unaonesha kwamba Wakenya wamegawanyika kuhusu hatma ya kisiasa ya Raila Odinga. Asimilia 35 wanamtaka astaafu siasani huku asilimia 26 wakihisi kwamba anastahili kusalia katika ulingo wa siasa ila asiwanie wadhifa wowote. Tom Wolf ni Mkuu wa Utafiti wa IPSOS.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.