×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Lulu Diva Single and Ready to Mingle Kenya

Living

Lulu Diva Single and Ready to Mingle Kenya Leo msanii wa bongo fleva kutoka Dar es Salaam amefunguka mengi kuhusu tasnia yake ya muziki ndani ya Konnect kupitia Radio Maisha. Lulu Diva mwimbaji wa kike mwenye kipaji cha aina yake amekiri wazi kwamba ilibidi aanzie na kuwa video vixen ili kujiongeza kwenye muzki wake. Ameonekana kwenye video mbalimbali za wasanii wa Tanzania ili kujifahamisha na kijitambulisha kwenye game huku akiongeza wadau wa kumpa support kwenye kazi yake. Akizungumza na watangazaji wa kipindi hicho, Mwende Macharia na Clemmo 254 amesema kuwa yeye huwa hakati tamaa akiamua kufanya kazi zake kwani mungu kampa uwezo na mikono ya kufanikisha. “Mimi huwa sikati tamaa mpaka kutimiza ninachotaka na tena huwa sipendi kiki za bure kama wasanii wengine wanachokifanya kwenye game” amefunguka pia kuhusiana na mahusiano yake na msanii madee baada ya kuonekana akimshikia nguo ndefu wakati wapo kwenye party ya msanii mkongwe wa bongo, Saida Karoli. Lulu ashawahi kuingia studio ndogo ndogo za mitaani kabla ya kupata sehemu yenye studio yenye ubora wa hali ya juu kurekod muziki wake. Mkali huyo wa ‘Utamu’ wimbo ambao una trend sana amezungumzia watu wanaopenda kufuatilia mambo ya watu kwenye ngoma hio kwani kila akifanya jambo nzuri wanamponda basi yeye anatoa utamu kwa wote wanaompa support sio wanafiki na wabaya wake. Hata hivyo suala la kuwahi kuandikiwa wimbo amezungumzia huku akisema kwamba ngoma yake ya ‘Milele’ aliandikiwa na msanii Barnaba Classic. Ciara na Rihana ni wasanii walimpa changamoto ya kufanya muziki wenye ubora kwani wamekuwa kama role model kwake pamoja na Ray C wa bongo fleva. Hatimaye mwende amehoji kama yupo na mchumba au boyfriend nay eye bila shaka ametoa ya moyoni. “Sina mchumba mimi wala boyfriend ila washikaji tu. Im single and ready to mingle Kenya” yeye kamaliza hivyo Diva wa ‘Utamu’

 

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles