×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

William Ole Ntimama azikwa Narok

Living

Na, Beatrice Maganga Hatimaye ibada ya wafu kwa aliyekuwa mwanasiasa mkongwe wa jamii ya Maasai, William Ole Ntimama imefanyika nyumbani kwake kwenye Kaunti ya Narok huku serikali ikiahidi kushughulikia dhuluma mbalimbali zilizotendewa Jamii ya Maasai. Katika hotuba yake, Rais Uhuru Kenyatta amesema serikali inafahamu fika masaibu ya jamii hiyo hasa hitaji la kuhifadhiwa kwa Msitu wa Mau na kuahidi kushughulikiwa kwa suala hilo ipasavyo. Vilevile amewataka wanasiasa kukoma kuingilia utendakazi wa serikali yake na badala yake kujiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao. Rais ametoa kauli hiyo baada ya viongozi waliotangulia kutoa hotuba zao akiwamo Kinara wa CORD Raila Odinga kuitaka serikali kuitekeleza ripoti ya Tume ya Ukweli, Haki na Maridhiano, TJRC kama ishara ya heshima kwa Ntimama aliyekuwa mstari wa mbele kupigania haki za jamii hiyo. Ripoti hiyo iliangazia baadhi ya dhuluma zilizotendewa jamii hiyo zikiwemo unyakuzi wa ardhi. Wito sawa na huo vilevile umetolewa na Kinara mwenza wa CORD Kalonzo Musyoka. Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Adan Duale hata hivyo amesisitiza kwamba ripoti hiyo iko mbele ya bunge na itajadiliwa. Wakati uo huo, Rais Mstaafu Daniel Arap Moi amemtaja Ntimama kuwa kiongozi aliyependa haki na muwazi. Akihutubu kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu wa matabaka mbalimbali, Kiongozi wa Upinzani nchini Tanzania, Edward Lowasa ametoa wito kwa jamaa wa Ntimama kumhudumia vilivyo mjane wa Ntimama, Dorcas Ntimama. Mazishi ya wanasiasa huyo mkongwe yamefanyika baada ya mahakama kulikataa ombi la mwanamume kwa jina George Karanja aliyewasilisha kesi kutaka yazuiwe hadi atakapotambuliwa na familia. Karanja alizuiliwa na polisi kuhudhuria mazishi hayo leo hii. Ntimama alifariki dunia Septemba mbili akiwa na umri wa miaka 86.  

 

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles