×
App Icon
The Standard e-Paper
Kenya's Bold Newspaper
★★★★ - on Play Store
Download Now
×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Ali Manzu: Buriani Kaka 'Daru' Darwesh

Living

Yaani hata sijui pa kuanzia. Hata hivyo, lazima nijikaze na kuandika yalo moyoni, licha ya machozi kunitiririka. Jamani Daru katuacha, bila kuaga. Hakika, sijawahi kufanya kazi na msimamizi wa aina hii.Anakukosoa na kukuelekezea kosa, kisha anakuonyesha njia ya kufuata ili kukuletea utatuzi wa kosa lako.

Alikua mcheshi, na si sifa sababu hayuko, bali alifahamika vyema na wenzetu hapa na hata katika afisi za mashinani. Walimuita Daru, labda ya kiwango cha hekima katika utatuzi wa mambo na kusuluhisha matatizo. Hakupenda kuegemea upande wowote katika utatuzi wa matatizo katika chumba cha habari, na wakati mwingine, alikua anachukua jukumu la kutwalii kesi kabla ya kuja na kutoa uamuzi. Alikua na busara ya hali ya juu.

Ahmed Darwesh hakuchagua wala kubagua. Daru, kama tunavyomuita, alikua mtulivu wa kusikiza na mchache wa kupapia kabla ya kuweka fikra zake kwenye mizani kisha azichururize kwa kukupa jibu.

Kisha kwa ucheshi, kuna majina ya kimajazi alipenda sana kutania wenzangu huku baada ya kukupa kibwagizo, huwa mwepesi wa kupiga hatua kiulaini na kusonga mbele huku akicheka, akikuacha nyuma ukitafakari. Ukarimu wake ulikua umevingirwa na imani ya kujali, kutoa, huruma na kichache alichokua nacho kwa wengine. Aisee, Mwenyezi Mteremezi aibariki na kuilinda familia changa alioiacha. Ni uchungu kuondokewa na mtu anayetegemewa, sio kwa familia yake pekee, bali jamii nzima. Changamoto inayonitia wasiwasi, ni je, nitaweza kuendeleza alichotuachia?

Kwa familia, jamaa, marafiki na hata mashabiki wa Daru, tupo pamoja. Tukumbuke Daru ameacha majukumu, letu ni kujizatiti kuwakumbuka japo kwa salamu. Hilo ndio litakalomfurahisha Marehemu aliko na hata kuimarika vyema kwa familia. Mungu tunaomba umueke pema penye wema ndugu Ahmed Juma Swaleh Darwesh. Amin.

Ali Manzu ni mwanahabari wa Ktn Leo aliyefanya kazi kwa ukaribu na mhariri mwendazake, marehemu Ahmed Darwesh. Wasiliana nae kupitia [email protected]; [email protected]

Jamii ya The Nairobian inachukua fursa hii pia kuomboleza na familia, marafiki na wafanyikazi wote wa shirika la The Standard Group.Tunaomba Mola amweke pema penye wema.

Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.

Marehemu Darwesh alikua mwandishi wa nakala ya Falsafa za Busara katika gazeti hili. Juma lijalo, tutachapisha nakala yake ya mwisho aliyowasilisha kabla ya kifo chake.

Buriani Kaka Daru.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week

.

Similar Articles

.

Recommended Articles