Gumzo la Wiki Podcast: UDA yadai kwamba kamatakama ya wanaohusishwa na chuki inawalenga wanachama wake, kunani? OKA nayo yaonekana kuchanganyikiwa kuhusu siku ya kumtangaza mgombea wa urais,
Published Jan. 15, 2022
00:00
00:00

Wanasiasa kadhaa wamekamatwa kwa kuhusishwa na matamshi ya uchochezi. Swali ni je, kuna mapendeleo jinsi UDA inavyodai? Je, ni kamatakamata kwa kigezo cha mirengo ili kuleta usawa wa kisiasa? Aidha, Rais Kenyatta alifanya mkutano katika Ikulu na viongozi wanaounga mkono Azimio la Umoja akiwamo Raila ambapo wote walipigia debe Mswada wa Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Kisiasa. Vigogo wa OKA walisusia mkutano huo wa Ikulu, licha ya kualikwa. Je, hatua yao inatoa picha gani?Vilevile, inadaiwa kwamba huenda Mudavadi akajiunga na Ruto, na Kalonzo kujiunga na Raila. Ikitokea hivyo, utapande gani utakuwa na nguvu? Masuala haya na mengine ndiyo yanayolipamba Gumzo la Maisha likiletwa kwako na wanahabari wetu, John Mbuthia akiwa Nyeri, Rose Mukonyo wa Machakos na Moses Kiraese wa Pokot Magharibi.