Siasa Podcast; Ni kwanini viongozi wengi hasa wawakilishi wadi wametemwa katika michujo za vyama?
Published Apr. 20, 2022
00:00
00:00

Mchujo wa vyama vya kisiasa unapoendelea, lipo jambo moja bainifu kuhusu matokeo kuhusu ngome za Naibu wa Rais William Ruto kulinganishwa na ngome ya Raila Odinga. Kwenye eneo la Bonde la Ufa ambako Ruto ana ufuasi mkubwa, baadhi ya wanasiasa wenye tajriba wamelambishwa sakafu huku vijana wengi wakiingia ulingoni. Na huko Nyanza, wanasiasa wengi waliokuwapo uongozini wamedumishwa hasa katika nyadhifa za ubunge, useneta na ugavana. Aidha, katika ngome zote mbili, idadi kubwa ya wawakilishi wadi waliokuwapo wamelambishwa sakafu na wapya kushinda tiketi. Hali hii inamaanisha nini kisiasa? Beatrice Maganga analiangazia suala hili.