Mwanajeshi mstaafu Marekani, anawania ubunge Marakwet Magharibi-Benson Cheserek
Published Jan. 18, 2022
00:00
00:00

Benson Cheserek ni miongoni mwa Wakenya ambao wanaishi ughaibuni (Kenyans in diaspora) na sasa analenga kuwania kiti cha ubunge kwenye eneo la Marakwet Magharibi katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet. Cheserek amekuwa akiishi Marekani kwa miaka 17 ambapo amefanya kazi katika jeshi la Marekani kwa miaka 8 kabla ya kuanza biashara yake binafsi. Kwenye mahojiano na mwanahabari Faith Kutere, Cheserek anasema analenga kutumia ujuzi wake katika idara ya usalama kusaidia kukabili ukosefu wa usalama kwenye Bonde la Kerio, kubadili maisha ya wakazi wa eneo la Marakwet Magharibi kupitia masomo miongoni mwa masuala mengine.