Ukweli wa Mambo: Mudavadi alisema ukweli Bomas ama la? Tunaweka paruwanja
Published Jan. 31, 2022
00:00
00:00

Katika Ukweli wa Mambo leo, tunaangazia hotuba ya Musalia Mudavadi wakati Kongamano la Kitaifa la ANC, Januari 23 mwaka wa 2022. Je, aliyoyasema yana ukweli ama la na kwa kiwango gani? Huu hapa ukweli wa mambo baada ya utafiti wa kina baina ya Shirika la Habari la Standard kwa ushirikiano na kampuni ya Africa Check. Katika hotuba yake ya kipekee ya kukubali uteuzi wa kupeperusha bendera ya urais kupitia chama chake, Musalia aliahidi kufufua uchumi jinsi alivyofanya alipokuwa Waziri wa Fedha miaka ya 90. Geoffrey Mung’ou anasimulia.