Rais Mteule William Ruto amekutana na Rais anayestaafu Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi.
Ruto ameandamana na mkewe Bi. Rachael Ruto kwenye mkutano ambao pia unahudhuriwa na mke wa Uhuru Bi. Margaret Kenyatta.
Mkutano huu unajiri siku moja tu kabla kuapishwa kwa Ruto kuwa Rais wa 5 akiwa na miaka 55.
Ruto ataapishwa Jumanne kwenye hafla itakayohudhuriwa na zaidi ya viongozi 20 wa mataifa mbalimbali.
Aidha, ujumbe wa Marekani na Uingereza utahudhuria kuapishwa kwa Ruto.
Rais Kenyatta anatarajiwa kumkabidhi rasmi mrithi wake mikoba ya uongozi.
Hafla hiyo itafanywa katika Uwanja wa Michezo wa Moi Kasarani.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.