×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Ruto azomewa na wananchi Kisumu

Living

Na, Cerel Mulindi/ Beatrice Maganga Ruto azomewa na wananchi Kisumu Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake, William Ruto wameizuru ngome ya mrengo wa NASA, Kaunti ya Kisumu huku msafara wao ukirushiwa mawe na wakazi waliokuwa wakiimba kusifu upinzani. Wawili hao walikuwa aneo hilo kuzindua miradi kadhaa ya maendeleo vilevile kuendeleza kampeni za kisiasa. Wakihutubu katika eneo la Ahero ambako Rais alizindua mradi wa kukarabati barabara kuu ya Ahero- Kisii, Rais Kenyatta ameisifu serikali ya Jubilee kwa baadhi ya miradi ambayo imewatekelezea wananchi. Naibu wake, William Ruto aidha amesema  serekali imejitolea kusambaza umeme nchini huku idadi ya walionufaika eneo hili ikiongozeka kutoka elfu 40 mwaka wa 2013 hadi elfu190, mradi ambao umegharimu kima cha  shilingi bilioni 1.2. Kwenye eneo la Okore ambako Rais amezindua mradi wa Kampuni ya East African Breweries wa ujenzi wa kiwanda cha pombe kwa kuweka jiwe la msingi, wakazi wamemzomea Naibu wake, William Ruto huku wakimzuia kuhutubia umma. Juhudi za Ruto kuwatuliza wakazi ziliambulia patupu na kumlazimu Rais kuingilia kati. Rais Kenyatta amesema ujenzi wa kiwanda hicho utachangia pakubwa ukuzaji wa uchumi wa taifa hili vilevile kubuni nafasi zaidi za ajira kwa wakazi. Rais aidha amezindua ujenzi wa kituo cha kupakia mafuta katika Ziwa Victoria ambacho amesema kitaanza kutumika kufikia mwezi Okotoba. Awali Rais amezindua rasmi Kivukio cha Mbita kwenye Kaunti ya Homabay kilichogharimu shilingi bilioni 1.5. Ujenzi wa kivukio hicho ulianza baada ya watu kadhaa kuaga dunia kwa kujaribu kuvuka Ziwa Victoria baina ya visiwa vya Rusinga na Mbita.  Wawili hao aidha wamewarai wakazi kuwapigia kura wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles