×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

RAIS AIDHINISHWA NA TUME YA IEBC

Living

Sophia Chinyezi Punde baada ya kuidhinishwa Rais Uhuru Kenyatta, Naibu Wake na viongozi wengine wa Chama cha Jubilee waliwahutubia wafuasi wao kwenye uwanja wa COMESA ulioko katika ukumbi wa KICC. Rais Kenyatta amewaomba kuipigia kura tena serikali yake wakati wa uchaguzi ili wakamilishe miradi ya maendeleo walioianzisha. Kadhalika amesisitiza umuhimu wa kuwaunganisha Wakenya wote ili kuzuia ghasia, umwagikaji damu na uharibifu wa mali, ilivyoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Aidha amesema serikali yake itawahudumia Wakenya wote kwa usawa bila ubaguzi. Rais ametaja baadhi ya ahadi zilizotimizwa na serikali, ahadi walizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2013. Kuhusu tatizo la baa la njaa Rais Kenyatta amesema walifanya wawezalo kuhakikisha unga mahindi unapunguzwa bei ili Wakenya wasiathike na njaa, huku akiahidi kwamba wametenga fedha zaidi za kuwashughulikia wazee pamoja na elimu ya wanafunzi wa darasa la kwanza hadi kidato cha nne. Kwa upande wake Naibu wa Rais William Ruto amesema Jubilee ina mpango wa kuhakikisha kwamba taifa hili linaimrika kwa kubuni nafasi za ajira kwa vijana, huku akisema upinzani hauna ajenda mwafaka kwa wananchi.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles