Kitakuwa kibarua kwa Uhuru na Raila kumzima Ruto 2022

Naibu Raisi William Ruto.

Kwa Raila Odinga, Uhuru Kenyatta ni “bwamdogo” kisiasa lakini je, kinganga cha wazee wanachokicheza mzimuni mwa William Ruto kitakesha ama kugeuka kinyafura cha watoto mtoni pepo za magharibi? Wamkumbusha kaa la baharini: macho utosini, mara mbele mara nyuma na hata ubavubavu fuoni bara na pwani ….. kkamba si kamba, baibui si baibui!

Sielewi kinacho wahangaisha dhidhi ya Naibu wa Raisi (Ruto) ilhali wana mbinu nyingi za kuzaliwa na kikatiba kumfurusha mbabe huyo wa Bonde la Ufa na kuunda jamuhuri  waitakayo na watakavyo nchini Kenya 2022. Swali; Je ni “Silaha ama fimbo zipi walizonazo bindoni Jubilee na ODM dhidi ya Ruto?

Na iwapo wanazo mahususi, je wana moyo wa paka na misuli ya farasi kuzitumia mwisho wa uwezo wao kumtia kigugumizi cha mwendo na mdomo William Ruto tofauti na silaha za zile za mwanzo zilioishia kumlewesha tu? Ama wanafungate hao wamezua tisha- toto kutufumba macho kwa “huwo huwo” za mwizi zisomaanisha kitu wala kutu?

Wakenya wameduwaa na vurumai hili lisiloisha kiasi cha kutabanga runinga, redio na msikio yao kila uchao huku njaa ikimaliza wakenya na ufisadi ukiendelea guu juu ya “Kibaki Tosha” mwishowe Raila kutupwa nje ya nusu makate ya NARC (National Rainbow Coalition)! Siasa haina adabu wala sharabu, bubu husema na kiziwi huskia. Ramli yangu inamuona Ruto kama kiongozi wa upinzani 2022 baada ya kukosa tikiti ya kigoro cha Uhuru – Raila, Ruto kivyovyote hatakubali, unaibu Raisi au chini ya hapo kwani atakacho ni “Raisi wa Kenya”.

Ni fukuto ambalo linatishia uchumi na hadhi ya Kenya ulimwenguni, siajabu, William Ruto majuzi aliitwa gumzo la faragha na balozi mmoja wa ng’ambo nchini. Waekezaji wa kimataifa hawapendi taharuki ama hali tata na sugu serekalini, gurudumu la soo la filisika na bidhaa ni kawanda lakustarehe kwa drafu la dola na reale wala si kashfa.

Tatizo ni kuwa hakuna mtu hata mmoja nchini Kenya awezae kujua Ruto atakuja na kichochoro gani mambo yakimharibikia. Uchu wake ni uraisi na hatamu za nchi hii mnamo uchaguzi mkuu ujao wa 2022; kula sahani moja kwa kiongozi wa upinzani Raila ?(ODM) na mdosi wake wa chama tawala cha Jubilee Alliance (Uhuru) kimeleta “mapinduzi baridi” ya watu wawili tu faraghani kiasi cha kuigeuza nchi nzima kuwa drafu la familia tatu kuu nchini – ile ya jomokenyatta, Daniel Arap Moi na Jaramogi Oginga Odinga. Ni uchunu wa mvuje kuhadaiwa avunje chama cha URP na kuungana na TNA (The National Party) cha Uhuru Kenyatta mnamo 2013 nakuweza kumrithi Raiai (Wakati huo) Mwai Emilio Kibaki.

Shart Ruto azinduke afahamu upepo umegeuka nchini:- yale mambo yakuchnagamyama nyungu na mivungu nakuteana kwenye kesi ya The Hague, uholanzi ambako yeye na Uhuru walituhumiwa kuchochea mauaji ya kikabila enzi za kibaki sasa ni maji yaliyomwagika hayazoleki. Uhuru Kenyatta wa leo alihitaji “kukubaliwa na Raila kama Raisi halali na Jamuhuri ya nne baada 2017 hivyo baada ya kutendeka hilo amepata mwandani mpya wakumaliza diba lake la pili uongozini.

Ruto kwa ufupi anekuwa gogo lililomvusha Uhuru akadhani ni dau kumbe ni kipande cha mbambakofi, ilivyo huenda marekebisho yatayo ya katiba 2022 yakamuwezesha waziri mkuu (Uhuru) kumteua Raila Raisi asiye mamlaka huku Joho, Kalonzo Musyoka na Gideon Moi wawe manaibu waziri mkuu.

Tusidanganyane Ruto na waitifaki wake serikali walijisahau nngwe hino wakafanya israfu serikalini ndiposa Uhuru Kenyatta akaonelea apasue jipu huenda jamaa wakatanabahi nakuacha kukorofisha nchi, tatizo ni kuwa hakuna ushahidi chuma uliotolewa ambako jina la William Ruto limetajwa, bado vitengo vya DCI (Directorate of Criminal Investigations) na kile cha maadili na ufisadi Ethics and Anti – corruption Commission (EACC) vimo nyanjani kubamba wavunjanchi! Noordin Haji mkurugenzi wa mashtaka ya umma (DPP) alituliza nyoyo za wakenya aliowaambia wand ishi wa habari kule Nairobi kuwa shilingi bilioni 16 za Kenya zimerudishwa mkoba wa serikali mfano “Hazina ya Bima ya Afya ya kitaifa mwenzake wa maswala ya Jumiya Afrika mashariki Adan Mohammed na Eugene wamalwa (wizara ya ugatuzi) pamoja na yule wa hazina kuu Henry Rotich wameitwa mbele ya DCI kujitetea.

Kwa Ruto, hata hivyo, hatua hizi ni njma dhidi ya waitifaki wake ama majogofyo tu yakufumba wakenya macho ilhali mapapa wengine wanaachiliwa. Ametumia janja kuu na tarafu ya ukabila huku akifika kuwa “ watu wetu” (wakalenjin) wanamaliz\wa.

Tuhuma za ufisadi ndio silah ya mwanzo kabisa ya Raisi Uhuru iliyomtia hasira na kiwewe Naibu Raisi. Siajabu kina Markomen na Oscar Sudi walimteremkia Gavana Hassan Joho wa Mombasa (Naibu mwenyekiti ODM) kwa tuhuma za mihadaharati lakini hakuna ushahidi wowote uliopatikana. Ikumbukwe, Joho ndiye jemedari mkuu wa Raila Pwani – na mshirika maendeleo wa Raisi Uhuru baada “handshake”.

Ni wazi raisi Uhuru na wandani washukiwa wa Ruto aliyowasopeka mamlakani kwenye mashirika na wizara za uma. Si ajabu baada Raila kumbatiza Ruto jina la “kuhani wa ufisadi” (High priest of Corruption), Ruto nae alimbandika (Raila) jina la “Bwana wa ufukara” (Lord of Poverty)!!

Ruto na wapambe wake pia wamebanwa kwa fimbo za wabunge na maseneta wa pande zote mbili – ODM na Jubilee. Mbinu hii ya serikali ya Uhuru inamuudhi sana Ruto kwani inampa sifa mbaya kila uchao kwenye vyombo vya habari na mitandaoni. Waswahili husema “ Kizuri hujiuza, kibaya hujitembeza”. Hii inamvurugia uaminifu na hadhi mbele ya wananchi na viongozi mashinani kwani “ndege wa rangi moja siku zote huruka pamoja”.

Washirika wengi wa Nairobi Raisi huyo wameshuka bei kisiasa akiwemo Aisha Juma, Moses Wetangula, Adan Duale, Katuo Ole Mitito, Markomen, Joyce Korir na (wakati mmoja) Mohamed Aor na Mwashetani na wengineo.

Mbali na mahakama na vyombo vya sheria vya dola, Raisi Uhuru amefanya mabadiliko ya msingi Baraza la mawaziri,Afisi za uma na Mashirika ya uma huku akiteuwa hata wandani wa viongozi wakuu wa upinzani Kalonzo Musyoka na Raila Odinga. Raila ametumia mbinu za nyanjani kumchafua Ruto kupitia majemedari wake ngangari James Orengo na Hassan Joho.

Aidha, mwenye kiti huyo wa ODM,kama Raisi Uhuru ameshamiri kumtupia William Ruto vijembe na mafumbo ya hapa na pale hasa baada ya ripoti ya watu kudhalilishwa na njaa Baringo, Bonde la ufa anako toka Ruto. Ni mbinu ambayo hupishana na ile ya “kimya”-hata kama Ruto na waitifaki wake wakimrushia madongo. La muhimu kwa Baba Tinga ni kuweka vigongo kila mkoa ili kumkera na kumtibua Naibu huyo wa raisi. Ni mbinu itakayo endelea hadi 2022.

Hivi karibuni Seneta James Orengo wa Siaya ametishia kupeleka mswada bungeni kumtimua Ruto kwa utovu wa nidhamu kwa kutoa matamshi kinyume na kauli ya Raisi Uhuru kuhusu ufisadi na uajibikaji. Sidhani mswada huo utapita kwani wana-Jubilee hawatakubali “mtu kando” amvue nguo kinara msaidizi wa chama tawala hata kama wao wenyewe wanampinga.

Labda mbinu ngeni ni “kusimamisha” wagombeaji uraisi watarajiwa 2022 mapemapema ili kuwarembaremba wapiga kura huku wakiwatumia kama sababu ya kuendelea kumponda Ruto na timu yake. Hassan Joho na Amason Kingi (ODM) wametangaza kugombea urais 2022 eti kuwakilisha wapwani na hadhi ya wapwani lakini cha ajabu ni kwamba tofauti na wenzao huko Bara wenye vyama vyao asilia (ANC ya Mudavadi, Wiper ya kalonzo n.k).

Magavana hawa hawana vyama vya kipwani na huenda wakajififiliza makusudi kama barafu wayeyuke jirani na uchaguzi mkuu wa 2022.Dawa ya moto ni moto; Hunda  Uhuru na Raila wakamtumia senetaGideon Moi wa Baringo kumkata makali Ruto kuelekea 2022. Si ajabu mwana huyo wa raisi mstaafu Daniel Arap Moi akafanywa naibu waziri mkuu katiba ikirekebishwa kabla hapo.

Mbinu nyengine ya Uhuru kuonyesha hakufuraishwa na nyendo za wateule wa serikali ni kuwapunguzia majukumu na hata vyeo kwa kuweka mteule mpya kwenye cheo cha kufikirika hapo kwa hapo. Mfano mzuri ni Naibu Raisi mwenyewe (Ruto) aliyekua “akitangatanga” mikoani (maneno ya Raisi) kufungua miradi ya maendeleo kumbe ni  kisingizio cha kujipigia debe kama Raisi mtarajiwa uchaguzi mkuu ujao.

Pwani alizoa wabunge 20 wakiongozwa na Dori na Jumwai Fred Matiang’i aliondolewa wizara ya elimu akawekwa ile ya usalama wa ndani kabla ya kufanywa waziri kiranja yana waziri kiongozi (chief minister) kusimamia na kushirikiza miradi yote ya serikali nchini na kuwajibisha mawaziri wengine ili Ajenda kuu 4 za raisi Uhuru zifaulu- Usalama wa chakula, Viwanda, Afya kwa wote na nyumba kwa umma.

Kimtazamo, Raisi Uhuru Kenyatta ni kama anamgeresha Naibu wake huyo asimuelewe afikiria nini hivi kwamba hata  majuzi Jumatano alimtembelea Ruto afisini mwake .Yanikumbusha enzi za Raisi mstaafu Daniel Arap Moi alivyompembapemba mkuu wa sheria nyakati hizo Charles Mugane Njonjo taratibu akamzonga ghafla alipomshtumu kuwa msaliti alieserikalini aliyetaka kumpendua.

Huenda Uhuru anapoesha joto la siasa dhidi ya Ruto ili nchi, serikali na uchumi wake usionekane uko hatarini mwa kutumbukia katika vurugo na sinto fahamu za kisiasa.Huku kwetu uswahilini, mbinu hii (ambayo tutaishuhudia sana kutoka upande wa Uhuru kuelekea 2022) inaitwa “Umma uvuviye” ama kwa king’weng’we,”Sticks and Carrots.”

La mwisho kwa William Samoei Ruto ; kwa nini aseme watu wake hivi sasa “wanamalizwa” lakini wakati walipoteuliwa nyadhifa hizo hakusema watu wetu “wanajengwa?”