×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Mwanapatholojia wa Serikali kuongoza upasuaji wa mili ya Shakahola

News

Shughuli ya upasuaji ya mili ya watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa mchugaji tata Paul Mackenzie iliyofukuliwa katika eneo la Shakahola kwenye Kaunti ya Kilifi inatarajiwa kuanza leo Ijumaa katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Malindi.

Idadi ya mili hiyo imekuwa ikiongezeka kila siku, huku  jana pekee mili mingine kumi na mmoja ikifukuliwa na kufikisha jumla ya mili,  mia moja na tisa.

Mwanapatholojia Mkuu wa Serikali Johansen Odour yu mjini Malindi kuongoza shughuli hiyo ambayo ilipaswa kuanza jana kabla ya kuahirishwa.

Hata hivyo kumekuwapo na mkanganyiko wa idadi ya mili inayofukuliwa tangu kuzuiwa kwa wnahabari na wanaharakati kufuatilia shughuli hiyo. Kamishna wa Eneo la Pwani Rhoda Onyancha aidha anasema hakuna aliyeokolewa katika oparesheni ya jana.

Familia zilizoripoti kutowekwa kwa wapendwa wao zikiendelea kufurika katika Hospitali ya Malindi kuwatafuta wapendwa wao miongoni mwa manusura waliokolewa kutoka kwenye msitu huo wa Shakahola.

Ikumbukwe Maafisa wa Idara ya Upelelezi DCI wanatarajiwa kuanzisha uchunguzi kwenye mali za Mackenzie baada ya mahakama kuipa idhini ya kuendeleza msako huo.

Haya yanajiri huku Naibu wa Rais Rigathi Gachagua na Mkewe Dorcus Gachagua wakikosoa kuendelea kushtumiwa kwa viongozi wa makanisa kufuatia kisa cha Mackenzie. Wawili hao wakisema mchungaji huyo anapaswa kuwajibishwa binafsi.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week