×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

DCI na IEBC waendelea kutofautiana kuhusu raia 3 wa Venezuela waliokamatwa

Maswali mengi yanaendelea kuibuka kuhusu raia watatu wa Venezuela ambao walinaswa wakiwa uwanja ndege baada ya kupatikana na makasa ya vibandiko vya uchaguzi katika hali tatanishi.

Haya yanajiri wakati ambapo Idara ya Upelelezi DCI imeendelea kuibua taarifa ambazo zinaashiria utata katika safari ya watatu hao kuja Kenya wakisemekana kuwa wafanyakazi wa kampuni iliyopewa kusimamia teknolojia.

DCI inasema watatu hao ambao mmoja wao ndiye amebainika kuwa mfanyakazi halisi wa Kampuni ya Kiteknolojia ya Smartmatic, walisafiri kuja Kenya wakiwa na pasipoti ambazo muda wa matumizi yao ulikuwa umekamilika.

Katika kurasa kumi na nne za taarifa katika mtandao wa Twitter,  DCI imeendelea kuibua maswali mazito kuhusu jinsi raia hao walivyosafirisha vibandiko vya IEBC kama mali binafsi, na kwamba walikuwa wakipeleka kwa nyumba ya mtu binafsi baada ya kupitia mataifa kadhaa badala ya kuja Kenya moja kwa moja. 

Bila shaka, Wakenya wangependa kufahamu ni vipi raia hao walivyopewa idhini ya kusafiri kutoka Venezuela kisha kuruhusiwa kuingia Kenya iwapo hawakuwa na pasipoti zinazotumika.

Suala jingine ni kwamba, wawili miongoni mwa raia hao wanasemekana kuwasili nchini Kenya mapema kabla ya mmoja wao kufika baadaye, kisha maafisa wa Upelelezi wa DCI kuwanasa.

Tangu alipoibua madai ya kusema maafisa wa usalama wanawahujumu wafanyakazi waliopewa kandarasi na IEBC ili kuendesha uchaguzi mkuu wa tarehe tisa mweziu ujao, bado Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati anasubiriwa kutoa majibu kufuatia maswali mengi ambayo yanaibuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Upelelezi DCI, George Kinaoti.

Wiki iliyopita, Chebukati na Afisa Mkuu Mtendaji wa IEBC Marjan Hussin Marjan walifanya kikao na wanahabari ambapo suala la utoaji kandarasi kwa kampuni ya Smartmatic lilitajwa kijuujuu.

Ni taarifa ambayo tunaendelea kuifuatilia katika chumba chetu cha habari, ikizingatiwa kwamba DCI imekuwa ikitoa taarifa kuhusu kila hatua ya uchunguzi unaoendelea.

Inaarifiwa kwamba raia hao watatu wa Venezuela, wametakiwa kujiwasilisha kwa Ofisi ya Kitengo cha Kukabili Ugaidi ATPU ili kuandikisha taarifa zaidi, huku wakili wao akisema serikali inapanga kuwafurusha.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week