×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Shariff Nassir ashinda ugavana wa Mombasa

Living

Abdulswamad Shariff Nassir ndiye Gavana Mteule wa Kaunti ya Mombasa.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa kwenye maeneo bunge mbalimbali Abdulswamad ameongoza kwa kupata jumla ya kura 119,083 na nshindani wake Hassan Omar akipata 98,108.

Kura hizo zinajumuisha maeneo bunge yote sita. Eneo Bunge la Likoni limekuwa la hivi punde kutangaza matokeo ya uchaguzi ambapo Abdulswamad amepata kura elfu kumi na saba, mia nne ishirini na tano huku mpinzani wake wa karibu Omar Hassan Sarai akipara kura elfu tisa mia saba hamsini na tano.

Kwenye kaunti ya Kakamega, matokeo ya uchaguzi yameendelea kuthibitishwa na kutangazwa.

Kufikia saa nne asubuhi, Mgombea wa ODM Farnandes Baraza alikuwa na jumla ya kura 95, 979 kulinganisha na mgombea wa ANC Cleophas Malala ambaye alikuwa na jumla ya kura 75,400.

Uchaguzi kwenye maeneo bunge ya Rongai kwenye Kaunti ya Nakuru, Pokot Kusini na Kacheliba kwenye Kaunti ya Pokot Magharibi, Kitui Rural vilevile kwenye wadi za Nyaki huko Meru na Kwa Njenga hapa Nairobi vilevile umekamilika.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles