×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

AMREF yashinikiza ushirikiano kufanikisha SDG'S

Living

Na Sophia Chinyezi Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la AMREF Dkt. Githinji Gitahi ameshinikiza kuwapo kwa ushirikiano katika utekelezaji wa Malengo Endelevu, SDGs. Kwenye mkutano wa wakuu mbalimbali jijini Nairobi, Amref imewasilisha mikakati itakayofuata wakati wa kutekelezwa kwa malengo hayo. Shirika hilo litashughulikia masuala manne muhimu miongoni mwa kumi na saba yaliyoorodheshwa; lishe na uzalishaji wa chakula, afya, usawa wa jinsia na uwapo wa maji safi na usafi wa mazingira. Mfanyabiashara Dkt. Manu Chandaria ambaye alikuwapo katika mkutano huo ametaja umuhimu wa ushirikiano huo ambao unaweza kusaidia kuwahamasisha wananchi ili kufahamu maana ya Malengo Endelevu. Mbali na kutoa fursa ya kufahamu anayehitajika kuhusishwa kwenye mpango huo, hafla hiyo imeashiria ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa ya Ajenda ya Afya Barani Afrika litakaloandaliwa Machi 7 hadi 9 mwaka ujao. Washirikishi mbalimbali watahudhuria mkutano huo, ambapo watajadili masuala mbalimbali ya afya, kubwa zaidi likiwa utekelezaji wa Malengo Endelevu kupitia kutiwa saini kwa mikataba na utangamano wa wafanyakazi wa afya katika jamii.  

 

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles