×
App Icon
The Standard e-Paper
Join Thousands of Readers
★★★★ - on Play Store
Download Now
×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Ayiro achukua hatamu chuo cha Moi

Living

Na Beatrice Maganga Licha ya pingamizi zilizoibuliwa na wanasiasa dhidi yake,  Laban Ayiro amechukua hatamu rasmi kuwa Kaimu Naibu Mkuu mpya wa Chuo Kikuu cha Moi,  kwenye hafla iliyofanyika katika bewa kuu mjini Eldoret. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Ayiro ametoa wito wa ushirikiano miongoni mwa washikadau wa chuo hicho ili kukiboresha zaidi. Kwenye hotuba yake ya kuondoka ofisini, aliyekuwa Naibu Mkuu, Richard Mibey amemtakia kila la heri mrithi wake. Siku ya Jumanne, Hapo jana  Magavana Jackson Mandago wa Uasin Gishu, Alex Tolgos wa Elgeyo Marakwet, wabunge James Bett wa Kesses na mwenzake wa Kapseret, Oscar Sudi miongoni mwa wengine walitaka kipindi cha kuhudumu cha Naibu Mkuu, Prof, Richard Mibey kuongezwa kwa wiki moja ili kutoa nafasi ya kumtangaza rasmi mrithi wake. Wanasiasa hao walitishia kusambaratisha hafla ya kufuzu kwa wanafunzi chuoni humo itakayofanyika kesho na Ijumaa iwapo malalamishi yao hayatazingatiwa. Wanasiasa hao wanataka mzaliwa wa eneo hilo, kupewa nafasi ya kukiongoza chuo hicho.  

 

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week

.

Similar Articles

.

Recommended Articles