×
App Icon
The Standard e-Paper
Truth Without Fear
★★★★ - on Play Store
Download Now
×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Serikali yaondoa ada za kulipia mitihani katika shule za binafsi

Living

Na, Carren Omae

Serikali imeondoa ada za mitihani katika shule za binafsi kote nchini. Rais Uhuru Kenyatta amesema wanafunzi watakaofanya mitihani ya kitaifa katika shule za msingi na upili katika shule hizo hawatahitajika kulipia ada zozote, sawa na wale shule za umma. Wakati uo huo, Rais Kenyatta amesema serikali haitatoa mwongozo mpya kuhusu karo za shule mwaka huu. Amesema jumla ya shilingi bilioni 29 zilizotolewa kufanikisha elimu bila malipo katika shule za kutwa za upili ziwatasaidia wanafunzi wengi kutositisha masomo yao kutokana na ukosefu wa karo. Kulingana na Rais, serikali itaendelea kutoa fedha za kutosha kufanikisha elimu nchini. Ameyasema hayo wakati wa hafla ya washindi wa mashindano ya muziki ya shule katika Ikulu ya Nairobi.

 

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week

.

Similar Articles

.

Recommended Articles