×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Raia wa Uchina Wavamiwa Narok

Living

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, ZAIDI ya vijana mia mbili wa jamii ya wamaasai wamewajeruhi raia kumi na wanne wa Uchina wanaofanya kazi katika mradi wa reli ya kisasa, SGR eneo la Narok.

Inaarifiwa kuwa vijana hao wamekuwa wakishnikiza kupewa ajira katika mradi huo bila mafanikio na hivyo kuwavamia raia hao wa Uchina kwa fimbo eneo la Duka moja kwenye barabara kuu ya Narok - Mai mahiu.

Polisi waliokuwa wakishika doria eneo hilo walilazimika kufyetua risasi hewani ili kuwatawanya vijana hao waliokuwa wamejawa na ghadhabu.

Shmabulizi la jana linajiri wiki tatu tu baada ya kundi lingine la vijana wasiopungua mia tatu kuandamana dhidi ya kampuni ya China Roads and Bridges ambayo imepewa kandarasi ya kufanikisha mradi huo wa reli ya kisasa, wakidai kunyimwa nafasi za ajira.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles