×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Ruto asema masomo yaendelee

Living

Na, Beatrice Maganga

Ruto asema masomo yaendelee hadi mwisho wa muhula huu

Licha ya wito wa kufungwa kwa shule za upili kupamba moto nchini ili kuzuia visa zaidi vya moto shuleni, serikali imesisitiza kwamba ni sharti masomo yaendelee hadi mwisho wa muhula huu. Naibu wa Rais William Ruto amesema mikakati inawekwa kuthibiti hali. Aidha kwenye mkutano uliowajumuisha Waziri wa Elimu Fred Matiang’i, viongozi wa dini na wale wa Muungano wa Wakuu wa Shule za Upili KESSHA, viongozi hao wamesema shughuli ya masomo zinaendelea katika shule nyingi nchini, hivyo hakuna haja ya shule zote kufunzwa. Baada ya kikao kilichochukua takribani saa tano, washikadau hao wameafikiana kwamba ratiba ya mitihani kwenye shule za upili itaendelea kama kawaida hadi shule zifungwe kwa mujibu wa kalenda ya elimu na kuelezea haja ya wanafunzi kikamilisha mitihani ya mwisho wa muhula kabla ya shule kufungwa. Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Nchini, Jackson Ole Sapit aliwasilisha taarifa kuhusu yaliyoafikiwa. Aidha imeafikiwa kwamba kamati iliyobuniwa kuchunguza chanzo cha mikasa ya moto shuleni iandae ripoti yake haraka iwezekanavyo na kuwasilisha mapendekezo kwa wakati. Makundi hayo yameafikiana kuandaa mkutano mwingine Septemba ishirini na tatu utakaowajumuisha washikadau mbalimbali wa elimu kujadili njia za kuboresha usimamizi wa shule. Akiwahutubia wanahabari baada ya kukihudhuria kikao hicho, Mwenyekiti wa Tume ya Uwiano na Utangamano wa Taifa Francis Ole Kaparo amesema visa vya moto katika shule za upili vinastahili kushughulikiwa ipasavyo. Mkutano huu unajiri siku moja baada ya Muungano wa Walimu Wakuu wa Shule za Upili KESSHA ambao umekutaka na Tume ya Huduma za Walimu TSC kwa siku ya pili leo, kuafikiana kwamba walimu wakuu na manaibu wao wazingatie sheria inayowataka kuishi katika makao ya shule. Kufikia sasa zaidi ya shule mia moja kote nchini zimeathiriwa na visa vya moto.?

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles