×
App Icon
The Standard e-Paper
Join Thousands of Readers
★★★★ - on Play Store
Download Now
×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Oswago Adai Kuhujumiwa na EACC

Living

Na, Beatrice Maganga Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi EACC, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali vilevile Kamati ya Bunge ya Uhasibu wa Umma, PAC zimeshtumiwa kwa kutofanya uchunguzi wa kina kuhusu chanzo cha kufeli kwa mashine wakati wa uchaguzi mkuu uliopita. Aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Uchaguzi EBC, James Oswago aidha amejitenga na madai ya kufujwa kwa fedha kupitia ununuaji wa mashine hizo jambo lililochangia kuibuliwa kwa sakata ya Chicken Gate.  Akizungumza siku baada ya Tume ya EACC kuwasilisha faili kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Keriako Tobiko ikipendekeza kushtakiwa kwake, Oswago amesema EACC haikumpa fursa ya kujieleza kuhusu ununuaji wa mashine za uchaguzi.Amesema kufeli kwa mashine hizo wakati wa uchaguzi mkuu kamwe hakukusababishwa na mchakato wa ununuaji. Wakati uo huo, Oswago ameikosoa Ofisi ya Mkaguzi MKuu wa Serikali kwa kutowahoji maafisa wengine waliohusika na ununuaji wa vifaa hivyo na kuandaa ripoti iliyodai kwamba sheria za shughuli hiyo ya ununuaji zilikiukwa. Hata hivyo amefichua kwamba IEBC ilinunua vifaa vya gharama ya juu ikilinganishwa na bajeti yake. Hapo jana, EACC ilimwondolea mashtaka Mwenyekiti wa IEBC Isaack Hassan, kuhusu tuhuma hizo huku ikipendekeza Oswago, ajenti Trevy Oyombra, Hamida ALi Kibwana na Kenneth Karani washtakiwe. Maafisa wa IEBC na wale wa Baraza la Mitihani Nchini, KNEC wanadaiwa kupewa hongo ya shilingi milioni 52 katika sakata hiyo. 

 

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week

.

Similar Articles

.

Recommended Articles