×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Anne Ngugi: Saa ndio maisha yako!

Living
 Kumbuka kuwa muda ukiyoyoma, basi hautaweza kuurejesha nyuma Picha: Hisani

Walosema kuwa ‘time is money’ (saa ni pesa) kamwe hawakukosea.

Ndio maana lazima ufanye kila sekunde inayogonga iwe na umuhimu katika maisha yako ya kila siku.

Maisha yetu kila wakati hutiwa katika mizani ya mudatunayotumia katika shughuli zetu. Yaani dhamani ya maisha yako hudhihirika kutokana na mtazamo na uzito wako wewe mwenyewe .

Ukiyachukulia maisha yako kwa wepesi wa karata za pata potea, basi utaambulia patupu.

Watu ambao wamefaulu katika miito ya maisha wanafahamu umuhimu wa kuheshimu masaa — na ni jambo ambalo wanalidhamini zaidi.

Watu hawa wanajua fika kuwa masaa ambayo hauyadhamini pia hayataongeza dhamana maishani mwako.

Basi kwenye ulingo wa maisha peupe nikiwa ninakunong’onezea kuhusiana na yale muhimu maishani nakusihi usije ukapuuza saa au muda wako lazima udhamini masaa yako.

Kumbuka kuwa muda ukiyoyoma, basi hautaweza kuurejesha nyuma ndiposa ufanye jambo fulani.

Nitaangazia mwandishi mmoja wa vitabu kutokana nchi ya Ufaransa ambaye ucheshi wake wa kuandika ni mithili ya uvumbuzi wa mambo kadhaa duniani. Mwandishi Marc Levy alipeana mtazamo wako kuhusu uratibu wa kutumia muda au masaa ya binadamu .

Marc akanena hivi: “...hebu tafakari kwamba kuna akaunti mmoja ya benki ambayo huwekwa kiasi cha dollar 86,400 yaani kiasi cha millioni 88 kila asubuhi. Siku inapoisha hakuna bakshishi zozote hukusanywa hadi siku ifuatayo na kila jioni benki ile hutupilia mbali fedha ambazo wewe hukutumia .je ungefanya nini kutumia fedha zote?”

Kila mmoja wetu anayo benki ile tuliyosimulia mwanzo..jina la benki ile ni masaa au muda wako, kila siku asubuhi hukupa sekonde 86400 ifikapo jioni masaa ambayo ulitumia ipasavyo yeye huiwekeza na masaa ambayo ulikaa hoi bila kufanya cha maana yeye huyatupilia mbali na yanakosa dhamana.

Hivyo, chochote ambacho unafanya wakati huu kinauhusiani mkubwa zaidi na maisha yako ya usoni.

Yaani itakuwaje upande mbegu za mahindi baada ya msimu wa mahindi ukatarajia kuvuna maharagwe ... lahasha

Hapa nchini kenya nimefanya kazi kama mtangazaji wa taarifa za habari kwa lugha ya kiswahili kwa takribani miaka 13.

Muda wangu mwingi kabla ya kunitazama kwenye runinga ulitumiwa kupiitia na kuhariri taarifa zile kwani ilipogonga saa mmoja kamili kama mwanahabari ningekuwa tayari kukupasha taarifa hizo ... na ndiposa nikashamiri katika sekta ya uanahabari .

Hebu sasa tutizame maisha ya mwanariadha yeyote yule kama mfano.

Tutumie mfano wa bingwa wa kimataifa wa mbio za masafa mafupi Usain Bolt kutoka nchini Jamaica. Bolt amekuwa bingwa katika mbio za masafa mafupi... lakini je wajua muda ambayo anatumia kufanya mazoezi ni asilimia 90 ya muda wake kabla ya mashindano hayo.

Hivyo, lazime tutumie muda wetu vyema ili kujianda kufaulu maishani. Ni sharti tutmie wakati wety vyema ili ifikapo wakati wetu wa kuiaga dunia, mwenyewe hautakuwa na bugutha kwani utajua uliyakamilisha yote kupitia muda ambayo ulipewa na Mola.

[email protected]

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles