Leo tutazungumzia magonjwa ambayo yanaweza kuwa hatari kwa wajawazito. Pumu, ugonjwa wa kisukari na kuwa katika hali ya kudhikika moyoni, vyaweza kudhuru afya ya mwanamke na mtoto wakati wa uja uzito kama hali hizo hazitashughulikiwa vilivyo. Mimba inaweza kusababisha hesabu ya chembe chembe nyekundu za damu kupungua na kusababisha ugonjwa wa anemia ambao una maana ya damu kupungua na kupata machovu na mwili kubadilika rangi na kuwa mweupe.