Mtalaa wa Umilisi, CBC unatarajiwa kukumbwa na changamoto hata zaidi baada ya walimu wakuu wa shule za upili kudai kwamba hawajahusishwa katika utekelezaji wake.
Akizungumza wakati wa Kongamano la 44 la Walimu Wakuu linaloendelea jijini Mombasa, Mwenyekiti wa Muungano wa Walimu Wakuu wa Shule za Upili, KESSHA Kahi Indimuli amesema walimu katika shule za upili hawana ufahamu kuhusu mtalaa huo mpya. Indimuli amesema serikali inapaswa kutoa mwanga wa iwapo mtalaa huo utatekelezwa katika shule za msingi pekee au hata upili.