Standard Digital News - Radio Maisha | Home
Kipindi cha sasa Maji Makuu

Baraza Kuu la Waisilamu Lataka Serikali Kuongeza Makataa

Baraza Kuu Waisalamu SUPKEM linaitaka serikali kuongeza makataa iliyotolewa kwa watu wanaoshirikiana na kundi la Al-shabaab kujisalimisha. baraza hilo linasema muda wa siku kumi haitoshi na kuihimiza serikali kuongeza makataa hayo kwa siku ishirini. Mwenyekiti wa baraza hilo Adan wachu aidha amesema serikali inafaa kuwahakikishia watakaojisalimisha usalama wao na kwamba msamaha unaotolewa na serikali uwe wa kweli. Kadhalika baraza hilo limependekeza kuwa wanaotaka kujisalimisha waruhusiwe kufanya hivyo kwa viongozi wa vijiji, mashirika ya kutetea haki za binadamu na viongozi wa dini. Kwa mujibu wa Wachu serikali inafaa kuweka mikakati ya kuwachunguza watu hao ili kuhakikisha maisha yao yanaimarika. Wakati uo huo, Kamishna wa kaunti ya Mombasa Nelson Marwa amesema watakaojisalimisha watapokea mafunzo mbalimbali ya kuboresha maisha yao. Akizungumza na wanahabari ofisini mwake, Kamishna wa Mombasa Nelson Marwa amesema vijana hao watasajiliwa katika Shirika la Huduma kwa Vijana NYS. Read More.....

Spika wa Seneti Azungumzia Suala la Kambi Ya Daadab

Spika wa seneti Ekwe Ethuro amesema serikali inafaa kushauriana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR kuhusu mipango ya kufungwa kwa kambi ya wakimbizi ya Dadaab. kihutubu kwenye hafla ya kufungua rasmi mkutano wa mabunge ya kitaifa ya kanda ya maziwa makuu, Ethuro amesema licha ya serikali kutaka kukabili magaidi nchini, usalama wa wakimbizi pia lazima uzingatiwe. Haya yanajiri wakati wakenya mbalimbali wameunga mkono mpango wa serikali kuifunga kambi hiyo ya Daadab. Ikumbukwe Naibu rais William Ruto alisema serikali haitalegeza kamba kuhusu mpango huo huku akisema serikali imeipa UNHCR makataa ya miezi 3 kuwahamisha wakimbizi hao hadi nchini Somalia.

Msanii Konshens aahidi kuja Kenya mwezi ujao

Anajulikana na wengi kama msanii aliyebobea Zaidi kwenye mtindo wa ‘Dancehall’. Pia, amewahi kuja nchini, lakini kulingana na mashabiki wake, hakuwatosheleza na wanahitaji kuburidishwa naye tena. Read More.....

Jay Z amtaja na Kumpongeza Lupita kwenye wimbo wake

Bila shaka, Lupita Nyongo amekuwa kioo cha jamii kufikia sasa, hasa katika maisha ya vijana nchini Kenya na Barani Afrika kwa jumla.

RATIBA YA KPL NA FKF

JUMLA ya mechi nane za kuwania taji la ligi ya KPL zimeratibiwa kupigwa wikendi hii. Read More.....

GOR MAHIA NJE YA BARA AFRIKA

TIMU ya Gor Mahia imebanduliwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Wakulima Watakiwa Kutafuta Njia Mbadala za Kuuza Mahindi

Bodi ya nafaka na mazao NCPB imewataka wakulima wa mahindi kutafuta njia mbadala ya kuuza mahindi yao. Meneja mkurugenzi wa bodi hiyo Newton Terer amesema bodi hiyo haina uwezo wa kununua mahindi yote kutoka kwa wakulima baada. Tere amsema tayari bodi hiyo imenunua gunia milioni 1.6 ya mahindi kutoka kwa wakulima Terer amesema hiki ni kiwango cha juu zaidi cha mahindi kuwahi kununuliwa na NCPB. Haya yanajiri huku mamia ya wkaulima wa mahindi wakihangaika kwa kukosa soko la mahindi yao baada ya NCPB kusitisha shughuli ya kununua mahindi hayo. Read More.....

Kiwango Cha Pesa Zilizotumwa Na Wakenya Chaongezeka

Kiwango cha pesa ambacho wakenya wanaoishi katika mataifa ya kigeni wametuma humu nchini kufikia mwezi February kimeongezeka kwa asilimia 11.6. Katika kipindi hicho jumla ya shilingi bilioni 11.6 zimetumwa nchini na wakenya hao. Kwa mujibu wa ripoti ya benki kuu ya Kenya asilimia 49 ya wakenya hao ni wakazi wa Marekani.Kwa mujibu wa ripoti hiyo jumla ya shilingi milioni 2.89 zimetumwa nchni na wakenya kutoka mataifa ya Uropa. Wakenya wanaoishi marekani walituma nchini jumla ya shilingi bilioni 5.62 huku wakenya kutoka mataifa mengine ya kigeni wakutuma jumla ya shilingi bilioni 2.83