Kijiji Cha Walemavu | Kisa Changu Podcast
Published Oct. 15, 2022
00:00
00:00

Kijijini Namawanga, kilichoko eneo la Busunu Kaunti ya Bungoma kuna takriban familia 27 hivi. Kisicho kawaida ni kwamba katika kila familia kuna angalau mtoto mmto mwenye ulemavu. Wapo waliozaliwa wakiwa na matatizo kuona, kuna wengine waliozaliwa bila viungo vya mwili kama vile miguu na mikono na wengine wana wanaugua ugonjwa wa seli mundu yaani sickle cell. Duncan Waswa amefika katika kijiji hicho na kuzungumza na baadhi ya wanakijiji. Haya hapa masimulizi yao ya kuvunja moyo.